Home » »

MKOA WA IRINGA WAJISIFU KWA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI MWAKA 2013

Wanahabari   wakiwa katika  kikao  hicho  leo
Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa  Dr  Christine Ishengoma  akizungumza na wanahabari  leo  juu ya utekelezaji  wa Ilani  ya uchaguzi kwa  mwaka 2013
Wanahabari  wa  vyombo  mbali mbali  wakifuatilia  kikao  cha  Rc  Iringa
Wakuu  wa  idara   wakiwa  katika  kikao  cha  mkuu wa  mkoa  na  wanahabari  leo
Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa  Dr  Christine Ishengoma  kulia  akieleza  jinsi ambavyo  mkoa ulivyotekeleza  ilani ya  uchaguzi kwa mwaka  2013

SERIKALI  ya  mkoa  wa  Iringa leo imetoa taarifa ya  utekelezaji  wa Ilani ya uchaguzi  kwa mwaka 2013 huku ikijivunia mafanikio makubwa ambayo yamefikiwa.

Akitoa taarifa   hiyo  leo mbele  ya  wanahabari  mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Dr Christine Ishengoma alisema  kuwa miongoni mwa mafanikio makubwa ambayo mkoa  wa Iringa  unajivunia ni katika sekta  ya  elimu, miundo mbinu, kilimo ,afya  na  nyingine nyingi.

Kwani  alisema  kuwa mkoa  umepiga  hatua  katika ujenzi  wa nyumba  za  walimu katika Halmashauri  zote za mkoa  wa Iringa lengo  likiwa ni  kuendelea  kuboresha  kiwango  cha  elimu  katika mkoa.

Akielezea  kuhusu  sekta ya afya  alisema kuwa hadi  sasa Hospital mbili  zinaendelea kujengwa katika manispaa na Kilolo pia  vituo  vya afya  na  nyumba  za watumishi  wa afya ikiwa ni  pamoja na kuendelea kusambaza  dawa katika vituo  vya afya.

Mkuu  huyo  wa mkoa  alisema  pia kumekuwepo na ufuatiliaji  wa huduma  zinazotolewa katika  vituo  hivyo na  Hospital .
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog