Home » »

Kauli ya Zitto Kabwe baada ya Kushindwa Kesi Aliyoifungua Dhidi ya CHADEMA.


Mahakama  Kuu ya Tanzania, leo imetupilia mbali shauri lililofunguliwa na Zitto Zubeir Kabwe mwaka jana, akipinga kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kumjadili, akikitaka chombo hicho cha sheria, kukielekeza chama chake, kusubiri kwanza rufaa yake aliyokuwa amekata katika Baraza Kuu.
 
Mahakama iliyoketi chini ya Jaji Mziray, ilikubaliana na hoja za mawakili wa Chadema, waliosema kuwa ufunguaji wa kesi hiyo ulikiuka baadhi ya vifungu vya sheria na hivyo kumtaka mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kulipa gharama zote za kesi hiyo.

Baada  ya  hukumu  hiyo, Zitto  Kabwe amesema  hakuwa  na wito wa mahakamani leo na  Jaji  aliyekuwa  akiisikiliza  kesi  hiyo amehamishiwa Tabora, hivyo  mwanasheria  wake  ameenda  kufuatilia  mazingira  ya  hukumu  hio.
 
"Hatuna taarifa ya Jaji Mpya. Mwanasheria wetu anafuatilia na atatoa statement", ameandika  Zitto  Kabwe  katika  ukurasa  wake  wa  twitter.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog