Home » »

..!! WANANCHI WALIOKUBWA NA MAAFA YA MVUA YA MAWE KAHAMA, WAFUNGA BARABARA YA KAHAMA KWENDA MIKOANI HADI SERIKALI IWAGAWIE MISAADA


Jinsi Magari yalivyozuiwa katika eneo hilo.

Abiria wanaokwenda mikoa ya Mwanza, Singida na Dar es salaam na Kwinginenko na wale wanaokwenda mikoa ya Kigoma na magari yote yanayokwena nchi jirani za Rwanda, Burundi, Uganda na Congo, wamekwama baada ya Wananchi wa kijiji cha Mwakata Kata ya Isaka wilayani Kahama kufunga barabara kuu ya kwenda maeneo hayo Aubuhi hii.

Taarifa kutoka eneo la Tukio zinasema wahanga hao wa janga la mvua ya mawe iliyouwa watu 46 na kujeruhi wengine zaidi ya 90, wameifunga barabara hiyo kuishinikiza serikali kuwapa misaada ya chakula na malazi, misaada ambayo imetolewa katika maeneo mbalimbali huku serikali ya eneo hilo ikiwa haijagawanya kwa wahanga husika.
Mpaka sasa tayari Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya kahama ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo Benson Mpesya ameshaenda eneo la tukio ili kuwasikiliza wananchi hao na kujaribu kumaliza tatizo hilo.


Hata hivyo taari tulizozipata hivi punde zinasema kuwa Tayari jeshi la polisi wilaya ya Kahama limefika katika eneo la tukio na kutumia mabomu ya machozi bila kuathiri wananchi na kufanikiwa kuwatawanya na kufungua barabara ambapo tayari magari yameanza kupita.

Ikumbukwe kuwa juzi Ahamisi Waziri mkuu Mizengo Pinda alikwenda kuzuru eneo hilo lililokubwa na maafa hayo kwa ajili ya kutolewa kwa misaada ya kibinaadam, ambapo pia mazao shambani na vyakula vilivyokuwa majumbani pamoja na mifugo vimeathiriwa.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog