Home » »

DOKII,NYAMIDELA,MASCO NA EZENICE KUPAMBA KAMPENI ZA UCHAGUZI KALENGA


[Image]
NA DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA

Aliyekuwa msanii maarufu wa maigizo ya kibongo, Ummy Wenslaus ‘Dokii’ ambaye kwa sasa anajishughulisha na sanaa ya muziki hasa katika mambo ya siasa ameahidi kuwepo mkoani Iringa katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge

Dokii aliyasema hayo juzi wakati aliposhiriki uzinduzi wa Mwaka wa Kilimo wa Afrika katika kijiji cha Kaning’ombe  kilichopo jimbo la Kalenga wilaya ya Iringa vijijini

msaani huyo alisema atashiriki kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge jimboni humo  huku akiahidi katika  kampeni hizo kusimama kwenye majukwa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kumpigia kampeni mgombea wake, Godfrey Mgimwa.

Kwa upande wake msanii anayeshughulika na kazi za chama cha mapinduzi ccm mkoa wa Iringa Damasi Masonda (Nyamidela) ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wa Godfrey Mgimwa washa moto kalenga alisema kuwa yeye kama msanii anayekitumikia chama hicho atahakikisha anafanya kampeni ya kumnadi Mgimwa katika jimbo lote la kalenga.

 Nyamidela ambaye alishawahi kuzunguka katika kampeni za urais mwaka 2010  amesema kuwa moto alioufanya katika kampeni hiyo na kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani mkoa wa Iringa ndio atakao washa katika jimbo la kalenga. 

Nyamidela ambaye ametamba na vibao kama face book, mautamu, kiambule, ccm jiwe kuu, nimepata mzuka wa kura vijana zai pamoja na wimbo nyamidela ambao ndio umebeba jina la msanii huyo.

aidha katika kampeni  hizo wasanii wengine mkoani humo wanaotarajia kumnadi mgombea Mgimwa ni msanii anayejulikana kwa jina la Emmanuel Mgata (Masco)  ambaye anatamba kwa kibao cha maisha magumu kijana pambana pamoja na  ezekiel Nice (Ezenice) anayeondoka kwa nyimbo za mchiriku huku akitamba kwa wimbo wa CCM chama bora.


uchaguzi huo utakaofanyika Machi 16, mwaka huu  umetokana  na  aliyekuwa mbunge wake Dk William Mgimwa kufariki dunia Januari 1, mwaka huu,

Katika uchaguzi huo mgombea wa ccm Godfrey Mgimwa atapambana na wagombea wa vyama viwili vya siasa ambavyo ni Chadema kilichomsimamisha mgombea Grace Tendega na Chausta kilichomsimamisha Richard Minja.

Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog