Home » »

DK SLAA KUZINDUA KESHO KAMPENI ZA CHADEMA UCHAGUZI MDOGO KALENGA, CCM KUANZA JUMAPILI

[Image]
Dk Slaa

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbroad Slaa kesho Jumamosi atazindua kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, wilayani Iringa katika kijiji cha Kalenga.
Kwa upande wao Chama cha Mapinduzi (CCM) kitanzaa kampeni zake keshokutwa Jumapili katika kijiji cha Mseke wakati kikiendelea na maandalizi ya uzinduzi rasmi wa kampeni hizo.
Uchaguzi huo unakishirikisha chama kingine cha Chausta kilichomsimamisha Richard Minja kupeperusa bendera yake.
CCM kwa upande wao imemsimamisha, Godfrey Mgimwa, huku Chadema ikiwa imemsimamisha Grace Tendega.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Iringa, Pudenciana Kisaka, jimbo la Kalenga lina jumla wapiga kura 85,051.
Akizungumza Katibu wa Chadema Iringa Vijijini, Felix Nyondo alisema Dk Slaa atawasilia mjini Iringa kwa gari mapema kesho katika mapokezi yatakayohusisha msafara mkubwa wa magari na pikipiki katika eneo la Ndiuka mjini hapa.
Mbali na Dk Slaa, Nyondo alisema wengine watakaokuwepo kwenye uzinduzi wa kampeni hizo ni Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Leman na viongozi mbalimbali wa chama hicho.
Alisema baada ya uzinduzi huo, Chadema itaendelea na kampeni za kila siku na kwa mujibu wa ratiba yao, kila siku watakuwa wakifanya mikutano 39.
Nyondo alisema katika kampeni hizo Chadema itatumia helkopta (chopa) tatu, magari 56 na pikipiki 80.
Alisema vyombo hivyo vya usafiri vitagawanywa katika kata zote 13 za jimbo hilo ili kufanikisha shughuli nzima ya kampeni zao.
Kaimu Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassana Mtenga alisema CCM kwa upande wake inaendelea na maandalizi ya uzinduzi rasmi wa kampeni zake.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog