Home » » BIBI HARUSI AGOMA KUOLEWA SIKU MOJA KABLA YA HARUSI, BWANA MACHOZI TUPU.. PILAU LADODA

BIBI HARUSI AGOMA KUOLEWA SIKU MOJA KABLA YA HARUSI, BWANA MACHOZI TUPU.. PILAU LADODA

KIMENUKA! Ikiwa ni siku moja tu kabla ya kufungwa kwa ndoa kati ya Zuhura Omari na Abdallah Salehe, katika hali isiyotarajiwa, mke mtarajiwa amekataa kushiriki tendo hilo la kheri licha ya taratibu zote kukamilika na kusababisha tafrani kubwa huko Buguruni Kwa Mnyamani jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita.

Ndugu wakiwa hawana la kufanya baada ya binti huyo kugoma kuolewa.

Tukio hilo lilitokea Mei 23, mwaka huu wakati ndugu wa mume walipokusanyika nyumbani kwa Abdallah tayari kwa shughuli, lakini wakalazimika kuondoka baada ya kuelezwa kuwa mwanamke amekataa kuolewa, ikidaiwa ni mara ya pili baada ya kufanya hivyo tena mwaka jana.

Shuhuda wa tukio hilo aliliambia Ijumaa kuwa baada ya kukataa mwaka jana, taratibu nyingine zote, ikiwa ni pamoja na mahari na zawadi ndogondogo zilipelekwa ukweni na ndoa hiyo ikapangwa kufungwa Mei 22, mwaka huu, lakini ghafla wakapata taarifa hizo za kushangaza.

Akizungumza na gazeti hili, mdogo wa mume mtarajiwa ambaye alipewa jukumu la kumwakilisha kaka yake kwenda kumchukua mke, aliyefahamika kwa jina la Salehe alisema hadi siku hiyo, walikuwa wameingia hasara kubwa, hivyo kutaka walipwe gharama zote walizotoa, ikiwemo mahari (450,000), kitanda, godoro, kabati na magunia ya mchele uliokuwa upikwe shughulini.

Mmoja wa wanafamilia wa bwana harusi.


Waandishi wetu waliokuwa eneo la tukio waliwashuhudia baadhi ya mawifi wakiwa katika sare zao za madela wakingojea muafaka wa harusi hiyo huku wengine wakiandamana hadi nyumbani kwa bibi harusi wakidai ufafanuzi zaidi.
Bi harusi ambaye aliomba asipigwe picha alikiri kuwa ni mchumba wa Abdallah kwa mwaka mmoja na alitakiwa aolewe Mei 23, mwaka huu, lakini aliamua kubadili msimamo akidai mchumba wake ni mtata kwani amekuwa akimtuhumu kutembea na mpemba mmoja (jina halikupatikana).
“Huyo Mpemba nilisoma naye sekondari, kwa sasa ni rafiki yangu wa kawaida. Nimegoma kuolewa kwa sababu mwanaume ni mtata sana.

Mmoja wa wanafamilia akiwasiliana kwa simu.


Binafsi nimeshindwa kwa sababu malengo yangu siyo niolewe leo halafu kesho nirudi nyumbani, nataka nikae na familia, tuzae tukiwa na amani na mume wangu, ila kwa huyu nimeshindwa, kama wameandaa pilau lao huko lidode tu,” alisema Zuhura huku mama yake akidai wamesharudisha baadhi ya vitu walivyopewa.

Jitihada za kuzungumza na bwana harusi hazikuzaa matunda ila jitihada za kumtafuta zinaendelea.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog