Home » »

Wateja wa Airtel kununua Tiketi za Ndege za Precicsion Air kupitia huduma ya Airtel Money

Meneja Uendeshaji wa pitiaAirtel Money Asupya  Naligingwa (kushoto) akiongea wakati wa uzinduzii wa ushirikiano kati ya Airtel na Precision Airt utakaowawezesha wateja wa Airtel kulipia tiketi za ndege kupitita huduma ya Airtel Money. akishuhudia ni Afisa uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde na na Afisa masoko wa Precision Air Hillary Mremi
 
Meneja Uendeshaji wa pitiaAirtel Money Asupya  Naligingwa (kushoto)  na Afisa masoko wa Precision Air Hillary Mremi (kulia) kwa pamoja wakizindua ushirikiano kati ya Airtel na Precision Air utakaowawezesha wateja wa Airtel kulipia tiketi za ndege kupitita huduma ya Airtel Money. akishuhudia ni Afisa uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde
 
Wateja wa Airtel kununua Tiketi za Ndege za Precicsion Air kupitia huduma ya Airtel Money
·         Wateja wa Airtel wawezeshwa kulipia tiketi zao za ndege kwa njia rahisi na haraka zaidi
 Dar es Salaam Jumatano , Mai 7, 2014, kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeanzisha ushirikiano na Precision Airtel utakaowawezesha wateja wake nchi nzima kununua tiketi za ndege kupitia huduma ya Airtel Money
Ushirikiano huu utawapatia wateja wa Precision Air urahisi katika kupanga safari zao na kuwawezesha kununua ticket zao wakati wowote bila usumbufu kupitia huduma ya Airtel Money.

Akionge wakati wa uzinduzi Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde alisema ushirikiano huu utawapatia wateja wetu wa Airtel  njia mbadala, rahisi naya uhakika ya kulipia safari zao za ndani na za nje  huku ikiwapatia watanzania na wateja wetu uzoefu tofauti wa kufanya malipo ya tiketi zao za ndege kupitia simu zao za kiganjani. 

 Kwa   kupitia huduma hii mpya  sasa wateja wetu wataweza kufanya malipo ya tiketi zao za ndege mahali popote kwa usalama  na haraka zaidi  kupitia huduma ya Airtel Money. ”

“Tutaendelea kuthibitisha dhamira yetu ya kutoa bidhaa na huduma za kibunifu huku tukiwahakikishia wateja wetu huduma bora kupitia huduma ya Airtel Money na nyinginezo wakati wote”. Aliongeza Matinde
Akiongelea  kuhusu ushirikiano huo Afisa Masoko wa Precision Air Bwana Hillary Mremi alisema “  

ushirikiano huu umekuwa kwa wakati muafaka wakati Precision  Air imejipanga kuboresha  huduma zetu na kuwapatia wateja wetu uzoefu tofauti katika huduma za ndege  huku tukihakikisha wateja wanafurahia huduma zetu zinazoenda zaidi ya matarajio yao.

Wateja wetu sasa wanaweza kufanya malipo ya tiketi zao za ndege  kwa kupitia huduma ya Airtel Money . kupitia simu zao za mkononi wateja wetu wanaweza kupiga call center au kutembelea tovuti yetu kufanya booking ya safari zao na kulipia kupitia Airtel Money na kisha kupokea tiketi yako kupitia simu yako ya mkononi” aliongeza Mremi

Akiongea kuhusu namna ya kupata huduma hiyo Meneja uendeshaji wa Airtel Money  Asupya  Naligingwa alisema” huduma hii ni rahisi kutumia , mteja anachotakiwa kufanya ni kupiga simu na kufanya booking ya safari au kufanya booking kupitia tovuti ya Precision Air ambapo mteja atapewa namba ambayo itatumika kama reference wakati wa malipo.

Kununua tiketi kupitia Airtel Money wateja wanatakiwa kufanya yafuatayo
Piga  *150*60#
Chagua namba  5  (Lipia Bili)
Chagua namba 8 (NYINGINEZO)
Andika jina la biashara
PW
Ingiza Kiasi  cha pesa
Kumbukumbu rejea
(namba ya booking)
Ingiza neno la siri kulipa PW, Tsh xxxxx, kumbukumbu rejea namba xxxxxx
Baada ya kufanya  hayo utapokea ujumbe wenye uthibitisho wa malipo na tiketi yake ya ndege “aliongeza Nalingingwa
Huduma ya Airtel Money ni huduma inayowawezesha wateja wa Airtel Nchi nzima kufanya malipo na miamala ya pesa kupitia pesa simu ya mkononi . kwa kupitia huduma ya Airtel money wateja wanaweza kulipia ankra  kama vile DAWASCO, LUKU, USA visa, DSTV, kulipia mikopo , kununua muda wa maongezi, kununua vifurushi vya yatosha na kutuma na kupokea pesa kutoka kwa marafiki na familia na huduma nyingine nyingi.
Mwisho
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog