Home » »

WAPENDA MIUJIZA, HIKI NDICHO KINACHOWAPATA

Mtume Lesego Daniel.
Leo bado tupo nchini Afrika ya kusini, kuhusiana na huduma ya mtume Lesego Daniel iitwayo Rabboni Centre ministries ambayo inaendelea kujizolea waumini kila kukicha licha ya aina ya ufunuo unaotumiwa na muasisi wa huduma hiyo mtume Lesego kuleta ualakini kama kweli umetoka kwa Mungu, hasa kitendo cha kuwataka waumini wake kula manyasi na majani ya miti lakini pia mda mwingine kuwafanyia maombi akiwa amewakanyaga.

GK imeamua kuandika tena hii leo kuhusiana na huduma hii, mara baada ya kuona video fupi iliyorekodiwa na mchungaji Thami Dlalisa wakati akiangalia kipindi kwenye runinga kilichokuwa kikionyesha huduma ya mtumishi Lesego akiwa amemrukia kwa juu kwa kumkanyaga kwa nguvu mwanadada aliyekuwa amelala chini kwa ajili ya maombi kitendo ambacho pia kilisikika sauti ya waumini wake ikionyesha mstuko namna dada huyo atakavyohimili uzito wa mchungaji huyo.

Katika maelezo yake mchungaji Dlalisa ambaye alirekodi video fupi ambayo ipo chini, amewataka marafiki zake wa facebook kuangalia video aliyorekodi yenye dakika 12 na kuwataka maoni yao wanafikiriaje watakachokiona, mchungaji anamrukia muumini wake wakati wengine wamesimama kama mazombi huku wengine wamekaa kama wanatazama igizo. Ambapo watu walioweka maoni yao walionekana kuponda sana huduma hiyo huku wengine pia wakisema hata waumini nao pia wanachangia kwa kupenda kufuata miujiza.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog