Home » »

ISRAEL HOUGHTON KUIMBA NCHINI UGANDA MWEZI UJAO, HAKUNA KIINGILIO

Watoto Children Choir namba 66 wakiimba kanisani kwao kabla ya kuelekea nchini Australia kwa ziara wiki mbili zilizopita.
Nyota wa muziki wa injili duniani Israel Houghton kutoka nchini Marekani anatarajiwa kuwa mwimbaji mwalikwa katika sherehe za kutimiza miaka 30 ya huduma ya kanisa la Watoto Uganda pamoja na miaka 20 ya huduma ya wanawake na watoto kupitia Watoto child care ministries zote zikiwa chini ya kanisa la Watoto ambalo umaarufu wake umetokana na kwaya ya Watoto children chini ya waanzilishi wa huduma hiyo Gary na Marilyn Skinner  zitakazofanyika mwezi wa sita nchini
humo.

Israel na kundi lake la New breed wanatarajiwa kuimba siku ya alhamis tarehe 5 katika kanisa la Watoto west tukio ambalo halitakuwa na kiingilio lililopewa jina la 'Watoto Big Party'. Hii itakuwa si mara ya kwanza kwa mwimbaji huyo kuimba jukwaa moja na Watoto children choir ambao amekuwa akikutana nao sehemu mbalimbali. Mwimbaji huyo atakuwa nchini Uganda wiki moja baada ya kumaliza tamasha lake kubwa la uimbaji litakalofanyika jijini London nchini Uingereza tarehe 27 mwezi wa tano akiwa na kundi lake kamili.

Haya kwa wale wapenzi wa mwanamuziki huyo, ni kujipanga nauli ya kwenda na kurudi na sehemu ya kufikia bila kusahau chakula, onyesho halitakuwa na kiingilio.

Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog