Home » »

PICHA KAMILI ZA TAMASHA LA PASAKA KUTOKA MWANZA, MALOPE AMALIZA

Malkia wa nyimbo za injili barani Afrika, Rebecca Malope.
Kwa wale ambao hawakufanikiwa kufika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kwenye hitimisho la Pasaka, basi fursa ipo kupitia hapa kuona namna matukio yote yalivyokuwa, ambapo muimbaji mkongwe wa nyimbo za injili kutoka Afrika Kusini - tena malkia wa nyimbo za injili barani Afrika, Rebecca Malope alifanikiwa kugusa mioyo ya watu, si tu kwa uimbaji, bali hata kupitia kwa kuwatia moyo kwamba Mungu anasikia pale umuombapo.

Sehemu ya watu waliokuwa wakiingia uwanjani hapo.
Sehemu ya wakazi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake.
Son of Tanzania, Ephraim Sekeleti kutoka Zambia
Katika tamasha hilo ambalo lilihudumiiuwa na waimbaji mbalimbali kutoka maeneo tofauti barani Afrika, lilikuwa na ugeni rasmi wa Mbunge wa jimbo la Sengerema, William Ngeleja, ambapo alisisitiza watu kuliombea taifa katika mchakato huu mgumu ambao unapitia wa kupata katiba. Na pia wakati hupohuo risala iliyosomwa kwa mgeni huyo rasmi na mojawapo wa waratibu wa tamasha hilo, Bwana John Melele, Mhe. Ngeleja ametakiwa kuwakumbusha wabunge wenzake kuwa pasipo Mungu hakuna kitakachowezekana, na hivyo wamtangulize.
BWANA asifiweeee, asema mgeni rasmi, mbunge wa jimbo la Sengerema, Mheshimiwa William Ngeleja.
Tukio la uzinduzi wa album ya muimbaji Grace pia lilifanyika ambapo mgeni rasmi alikiri wazi kuwa amani ya Tanzania pia inachangiwa na waimbaji wa nyimbo za injili, na hivyo wanatakiwa kusonga mbele bila kukata tamaa.

Wachungaji wakiwa wameiwekea mikono album ya mwanadada Grace Mwikabwe
Rebecca Malope na timu yake wakiingia ndani ya uwanja tayari kwa kuhudumu.
Akipokulewa na baadhi ya waimbaji wenzake.
Timu ikiwa 'standby'

Sasa tayari kwa kazi

BOMU LALIPUKA NDANI YA KANISA LA KILUTHERI MWANZA NA KUJERUHI

Mhudumu wa nyumba ya kupumzikia wageni wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa Victoria, jijijini Bernadetha Alfred (25) akiwa amelazwa katika Hospitali ya Bugando baada ya kulipukiwa na Bomu hilo jijini Mwanza.
Mhudumu wa nyumba ya kupumzikia wageni wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa Victoria, jijijini hapa, amejeruhiwa vibaya baada ya kulipukiwa na bomu lililokuwa limewekwa kwenye korido la nyumba hiyo.

Tukio hilo lilitokea siku moja baada ya tamasha la kimataifa la pasaka kufanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba (Jumatatu), kati ya saa 1:45 na saa 2:20 usiku, katika eneo la Makongoro
wilayani Ilemela wakati mhudumu huyo Bernadetha Alfred (25) alipofungua kifurushi cha mzigo alichodhani kimesahaulika kwenye eneo hilo, kabla ya kumlipukia.

Kwa mujibu wa Katibu wa Dayosisi hiyo, Mollel Rogart, kifurushi hicho kilichokuwa kwenye mfuko mweusi wa nailoni, kilikuwa juu ya kreti (tupu) za soda, karibu na eneo la kulia chakula lililopo katika nyumba hiyo.

“Ule mfuko ulikaa pale siku tatu ndiyo usiku huo mhudumu wetu akakichukua kukiangalia akidhani ni mzigo wa mtu umesahaulika.” Alieleza Katibu huyo na kudai kuwa kifurushi hicho kilimlipukia mara tu alipokifungua na kujeruhi vibaya katika sehemu mbalimbali za mwili.

“Bernadetha kajeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo miguuni na usoni na siwezi kusema kwamba chanzo cha mlipuko huo ni mambo ya kidini japo ulinzi wetu haukuwa mkali kiasi cha kudhibiti watu walioingia na vitu.” Alisema

Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Valentino Mlowola akithibitisha tukio hilo, alisema kwamba uchunguzi wa awali uliofanywa na kikosi maalum kutoka Dar es salaam umebaini kuwa bomu hilo limetengenezwa kienyeji.



“Bado tunaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili tubaini ni nani kafanya ili kama ni mtu au kikundi kimehusika tuchukue hatua haraka. Natoa wito kwa wananchi kutochukua vitu ambavyo hawa uhakika navyo, wanapoona vitu vya aina hiyo, watoe taarifa kwetu.” Alisema Kamanda Mulowola.

Mlowola alieleza kuwa, Bernadetha aliyejeruhiwa vibaya katika sehemu mbalimbali za mwili, alikimbizwa katika Hospitali ya rufaa ya Bugando ambako anaendelea na matibabu.

Kamanda huyo alieleza kwamba, mabomu (yakiwemo ya kienyeji) yako katika mifumo mbalimbali hivyo wananchi hususan wahudumu wa sehemu za mikusanyiko wawe na tahadhari na vitu vinavyoonekana kusahaulika na wasisite kuwajulisha polisi vinapoonekana hivyo.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog