Home » »

WAPENZI WA MUZIKI WA GOSPEL JIJINI NAIROBI KUKUTANISHWA NA PAUL MWAI

Paul Mwai mwandaaji wa tamasha hilo.                   
Wapenzi wa muziki wa gospel jijini Nairobi nchini Kenya wanatarajiwa kukutanishwa pamoja siku ya tarehe 2 mwezi ujao katika uwanja wa mpira wa Thika kwenye tamasha kubwa la muziki wa injili lililoandaliwa na mwimbaji aliyejipatia umaarufu siku za karibuni Paul Mwai ambaye ameamua kulipa jina  tamasha hilo kama  Groove awards skiza tune of the year celebration.

Mwimbaji huyo ambaye amefahamika zaidi nchini kwa album yake ya Racing Up amewaalika waimbaji mbalimbali kutoka nchini humo akiwemo Emmy Kosgei, Mbuvi, Pastor Ruth Wamuyu, Ben Githae, Loise Kim, Carol Wanjiru, Charles Kingori, James Warachi, Muigai Wanjoroge na waimbaji wengine wengi huku waendesha tamasha hilo ama MC bwana Mwai amewataja kuwa ni Muthee Kiengei akisaidiwa Olo Matope wa Coro Fm.

Tanzania imekuwa ikisifika katika nyanja ya muziki kwa ujumla nchi za Afrika ya mashariki ikifuatia Kenya lakini pia katika uchunguzi uliofanywa na GK kwakusikiliza maoni ya watu mbalimbali inaonekana kwamba licha ya Tanzania kuwa juu, lakini waimbaji wa nchini Kenya wameonekana kufanya kazi zao katika viwango vya juu katika recording audio pamoja na video hali ambayo ni tofauti na waimbaji waliowengi nchini ambao linapokuja suala la ubunifu katika kazi zao haswa video mara nyingi muongozo(script) unakuwa mbaya.
Paul Mwai katika moja ya huduma zake za kumwinua Mungu.              
Emmy Kosgei kuongeza nguvu katika tamasha hilo.   
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog