Home » »

KWA TAARIFA YAKO--WADOGO ZAKE UCHE WOTE WAFUATA NYAYO ZA WAZAZI ''WACHUNGAJI''

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu cha ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu
Pastor Uche akiwa na mdogo wake anayemfuatia Pastor Samuel Bruno.
Ninadra sana kukuta familia ya watoto zaidi ya mmoja kufuata nyayo za wazazi wao wote kwa pamoja ama kama baba ni docta basi watoto wote wanakuwa madokta, basi KWA TAARIFA YAKO ni kwamba mwimbaji aliyejitambulisha vyema na wimbo wake wa ''My God is good'' kupitia kundi la Joyous Celebration pastor Agu Uchechukwu a.k.a Double double ambaye ni mtoto wa kwanza kuzaliwa katika familia yao ya watoto watano wa mchungaji Bruno.

Uche ambaye alibarikiwa mwaka 2010 kuwa mchungaji kupitia Alleluia Ministry ya Afrika ya kusini, mdogo wake anayemfuatia Samuel Bruno ni mchungaji ambaye amefungua huduma yake jijini London nchini Uingereza ikifahamika kwa jina la Hopeway Ministries International, huku wadogo zake kama Miracle Bruno, Chisomi Bruno wenyewe wako nyumbani Nigeria na wazazi wao wakitumika katika makanisa mbalimbali wakifahamika kama wainjilisti hata Uche alithibitisha hilo wakati alipofanyiwa mahojiano na Wapo Radio Fm siku zilizopita
.
                  


MY GOD IS GOOD EVERYTHING DOUBLE DOUBLE
Wimbo huu ndio uliompa Uche tiketi ya kujiunga na Joyous mwaka 2009 baada ya mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Maduhva aliyekuwepo katika kanisa la Rhema North aliposikia mwimbaji huyo akiimba wimbo huo nakuupenda nakuamua kumtafuta mmoja wa viongozi wa kundi la Joyous bwana Lindelani Mkhize(choir master) ambaye aliamua kumwalika Uche kwenye mazoezi yao na kuanza kuufanyia mazoezi wimbo huo hatimaye kurekodiwa na Uche milango kuanza kufunguka nasasa anashiriki na waimbaji wengine wa kimataifa wa injili jukwaa moja.

Pamoja na hayo mwimbaji huyu lengo lake lilikuwa awe mwanasheria hakuwahi kuwaza kuja kuwa mwimbaji ingawa alipokuwa mtoto alikuwa akiimba kwaya ya watoto, amesema wazazi wake hawajawahi kumlazimisha kumwamini Mungu ama kuwa mwimbaji bali walikuwa wakimuombea mpaka Mungu alipomuonyesha wito wake katika maisha ambako anasema kwakweli ana kila sababu ya kumshukuru Mungu mambo yanakwenda vizuri.
Wazazi wa pastor Uche.

Uche akiwa na wadogo zake waishio Nigeria alipowatembelea mapema mwezi May mwaka huu.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog