Home » »

MAMBO YAZIDI KUNYOOKA KWA WAIMBAJI WA GOSPEL NCHINI

Mwimbaji nyota wa muziki wa gospel nchini ambaye mashabiki wameamua kumpachika jina la malkia wa muziki wa gospel nchini bibie Rose Muhando kwasasa yuko busy nchini Afrika ya kusini akirekodi video ya album yake mpya ambayo hata hivyo jina bado halijatajwa ingawa GK inahisi album hiyo itaitwa Haleluya Hossana.

Akiwa chini ya kampuni maarufu ya muziki duniani ya Sony Music kwa barani Afrika ikiwa imejikita nchini Afrika ya kusini, tayari mwimbaji huyo alishakamilisha album ya sauti wiki mbili zilizopita na kwasasa tayari ameanza kurekodi nyimbo zilizobaki katika video yake hiyo ambayo inategemewa kuleta kitu cha tofauti kuanzia usikivu wa kanda bya sauti mpaka video kutokana na ubora wa kampuni hiyo ya Sony.

Rose Muhando katika pozi la picha.
Wakati huohuo mwimbaji mwingine wa muziki wa gospel nchini Upendo Nkone ambaye ameachia album yake ya nne hivi majuzi, jumamosi hii anatarajiwa kuwa mmoja kati ya waimbaji watakaomsifu Mungu katika tamasha kubwa la kimataifa  liitwalo ''International Gospel Music Festival'' litakalofanyika huko Columbus Ohio nchini Marekani likiwa limeandaliwa na Pastor Donis na mkewe Nnunu Nkone.

Hii itakuwa mara ya pili kwa Upendo kuingia nchini Marekani kwa ajili ya huduma ya kumtangaza Kristo ikitanguliwa na safari ya kwanza aliyokuwa ameambatana na waimbaji wenzake Upendo Kilahiro pamoja na Christina Shusho mwishoni mwa mwaka jana, ambapo tayari mwimbaji huyo ameshawasili nchini Marekani na kulakiwa na wenyeji wake.
Upendo Nkone akipokewa uwanjani mara baada ya kuwasili nchini Marekani.

Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog