Home » »

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU TAG, MAJAMBAZI WAVAMIA MAKAO MAKUU, WAHARIBU VITU NA KUIBA LAPTOP 3

Kanisa la TAG likiwa linajiandaa na uchaguzi wa nyadhifa mbalimbali unaotarajia kufanyika Dodoma, watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wamevamia ofisi za kanisa la TAG makao makuu na kuiba, usiku wa kuamkia Jumanne.

Taarifa zilizoifikia blog hii watu hao walivamia juzi usiku na kuwafunga kwa kamba walinzi waliokuwa zamu na hatimaye kuvunja ofisi mbali mbali za makao makuu ikiwemo ya askofu mkuu na kuharibu samani.
Askofu Mkuu wa TAG, Barnabas Mtokambali

Watu hao waliweza kufanikiwa kuiba laptop 3 katika ofisi hizo na hatimaye kuhamia ofisi za kanisa la TAG Ubungo ambako walifanya uharibifu na kufanikiwa kuiba sefu ya pesa, inayokadiriwa kuwa na kiasi cha shilingi milioni 6 za ujenzi wa kanisa, mafungu ya kumi na sadaka ambazo kiasi chake bado hakijafahamika.

Habari zaidi zinasema baadae sefu hiyo ilitelekezwa maeneo ya Kigogo na ikiwa limevunjwa na kuchukuliwa pesa yote.


Pamoja na wizi huo lakini leo ndiyo baadhi ya wajumbe wanaendelea kwenda katika mkutano mkuu wa kanisa la TAG unaofanyika Dodoma ambako kufanyika uchaguzi wa nyadhifa mbalimbali.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog