Home » »

KAMBI NA TAMASHA LA WAIMBAJI WA MKOA WA KIGOMA LAFANA

Wiki iliyoisha kuanzia tarehe 15 hadi 19 kumefanyika kambi pamoja na tamasha kubwa la waimbaji wote wa mkoa wa Kigoma(Leka Dutigite), tukio hilo ambalo limefanyika kwa mara ya kwanza na kwa mafanikio makubwa liliandaliwa na kwaya ya KYGC ya kanisa la Free Pentecostal Church Tanzania (FPCT).
Ambapo kambi imefanyika katika viwanja vya kanisa la FPCT Mwanga na kuhitimishwa kwa tamasha kubwa katika uwanja wa Lake Tanganyika likisindikizwa na waimbaji waliopo mkoani hapo na wale waishio nje ya mkoa huo kama Victor Aron, Upendo Nkone, Amon na mkewe Upendo Kilahiro, Mery Nkwabi na kwaya ya Dar es salaam Gospel Choir(DGC) kutoka FPCT Kurasini.

Kwa upande wa walimu waliohudhuria na kufundisha katika semina hiyo ni pamoja na George Mwita, Sossy Mabele, Joseph Malumbu pamoja na mwenyeji wao Wilson Gwimo, huku wahudhuriaji walilipa ada ya ushiriki katika kambi na tamasha hilo.
                                       ANGALIA BAADHI YA PICHA ZA TUKIO HILO.
Asubuhi watumishi wakipata kifungua kinywa kabla ya kutumika.
DGC wakimsifu Mungu kanisani Mwanga.
Amon Kilahiro wa kwanza kuume akiwa na watumishi wenzake.
Kwaya wenyeji waandaaji wa kambi na tamasha hilo KYGC wakimsifu Mungu.
Mmoja wa masolo matata wa DGC aitwaye Rose wa kwanza kuume akiwa na wenzake wakifuatilia kilichokuwa kikijiri madhabahuni.
Upendo Kilahiro akiwaongoza wenzake na Zindonga ziwelale.
DGC wakimsifu Mungu uwanja wa Lake Tanganyika katika tamasha.
Furaha ndani ya Yesu, DGC wakimsifu Mungu katika uwanja wa kanisa FPCT Mwanga.
Kiongozi wa kwaya ya DGC akipokea cheti cha ushiriki wa kwaya katika kambi na tamasha hilo.
DGC wakipanda gari kurudi kambini kujiandaa na safari ya kurejea jijini DSM.
DGC wakitoka uwanja wa Lake Tanganyika. Picha kwa hisani ya Eliud Mathias.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog