WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM KUKUTANA IJUMAA HII Wakazi wa jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake ijumaa hii wanatarajiwa kujumuika pamoja katika mkesha mkubwa wa maombi na maombezi unaotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa BCIC Mbezi beach uliochini ya Wapo Mission International na kiongozi wake askofu Sylvester Gamanywa. Mkesha huo ambao unatarajiwa kuwa na vipindi mbalimbali vya kusifu na kuabudu pamoja na neno la Mungu pamoja na maombi umekuwa ukivutia maelfu ya wakazi wa jiji hilo kutokana na kile ambacho Mungu amekuwa akitenda kupitia watu wake.Ambapo maombi maalumu yatafanyika...
mwimbaji wa mahiri wa nyimbo za injili NESTER SANGA KUZINDUA ALBAM YAKE MPYA IITWAYO TWENDENI. Mwimbaji Mahiri wa nyimbo za injili Tanzania kutoka Dar el Salaam Nester Sanga ameweka wazi malengo ya uzinduzi wa albam yake mpya jijini Mwanza iitwayo Twendeni ambayo ina takribani nyimbo tisa na imetoka mwezi huu wa nane.Akiongea na mwandishi wa habari hizi bi. Sanga amesema kuwa amefikia uamuzi huu baada ya kupata simu nyingi kutoka Mwanza watu wakimuomba aje afanye tamasha la uzinduzi wa albam yake mpya iitwayo Twendeni. Akizungumzia ubora wa albam hii ya Twendeni bi. Sanga amesema...
MAMBO YAZIDI KUNYOOKA KWA WAIMBAJI WA GOSPEL NCHINI Mwimbaji nyota wa muziki wa gospel nchini ambaye mashabiki wameamua kumpachika jina la malkia wa muziki wa gospel nchini bibie Rose Muhando kwasasa yuko busy nchini Afrika ya kusini akirekodi video ya album yake mpya ambayo hata hivyo jina bado halijatajwa ingawa GK inahisi album hiyo itaitwa Haleluya Hossana. Akiwa chini ya kampuni maarufu ya muziki duniani ya Sony Music kwa barani Afrika ikiwa imejikita nchini Afrika ya kusini, tayari mwimbaji huyo alishakamilisha album ya sauti wiki mbili zilizopita na kwasasa tayari ameanza kurekodi...
VIONGOZI WA DINI CHANZO CHA MIGOGORO--JAJI MKUU MSTAAFU Jaji mkuu mstaafu wa Tanzania akizungumza. Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustino Ramadhani, amewataka viongozi wa dini kuacha kuwa chanzo cha migogoro makanisani na badala yake kurudi zaidi kwa Bwana Yesu ili kuweza kutimiliza kusudi walilopewa katika utumishi wao. Rai hiyo aliitoa juzi siku ya Jumapili katika sherehe za uzinduzi wa miaka hamsini ya Umoja wa Kujisomea Biblia (Scripture Union) zilizofanyika katika ofisi za makao makuu ya shirika hilo maeneo ya Muhimbili wakati alipohudhulia kama mgeni rasmi wa tukio hilo. Alisema...

MJI MPYA WA WILAYA YA KILOLO HUENDA SASA UKAWA MOJA KATI YA MIJI BORA MKOA WA IRINGA KUTOKANA NA MAJENGO YANAYOENDEREA KUJENGWA

MJI MPYA WA WILAYA YA KILOLO HUENDA SASA UKAWA MOJA KATI YA MIJI BORA MKOA WA IRINGA KUTOKANA NA MAJENGO YANAYOENDEREA KUJENGWA
HII NI MOJA KATI YA GUEST NA LORGE MAALUFU UKIFIKA KATIKA WILAYA MPYA YA KILOLO KATIKA MKOA WA IRINGAA AFISA MTENDAJI WA KIJIJI CHA LUGANGA WILAYA YA KILOLO BWANA THABIT JUMA KALOLO AKIFAFANUA JUU YA UELEWA WA WANAICHI KUHUSU KATIBA MPYA HII NDO KATIBA YENYEWE mtangaji wa overcomers na mmiliki wa mtandao huu akifanya mahiojiano na baadhi ya wanaich...
MIRIAM LUKINDO, CHRISTINA SHUSHO KUPAMBA UZINDUZI WA ALBUM YA KWAYA Miriam Lukindo wa Mauki akimsifu Mungu. Mwimbaji wa muziki wa Injili nchini, Miriam Lukindo Mauki ‘Binti Afrika’ Jumamosi hii anatarajiwa kuiteka Matembele ya Pili, Ukonga jijini Dar es Salaam atakaposhiriki uzinduzi wa albamu mbili za kwaya ya Sauti za Sifa iliyo chini ya Huduma ya The Word of Reconciliation Ministries (WRM).Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwalimu wa kwaya hiyo, Elibariki Isango, alisema, Miriam amekubali kuungana nao na siku hiyo atapanda jukwaa moja na Christina Shusho kuimba, wakati...
KAMBI NA TAMASHA LA WAIMBAJI WA MKOA WA KIGOMA LAFANA Wiki iliyoisha kuanzia tarehe 15 hadi 19 kumefanyika kambi pamoja na tamasha kubwa la waimbaji wote wa mkoa wa Kigoma(Leka Dutigite), tukio hilo ambalo limefanyika kwa mara ya kwanza na kwa mafanikio makubwa liliandaliwa na kwaya ya KYGC ya kanisa la Free Pentecostal Church Tanzania (FPCT). Ambapo kambi imefanyika katika viwanja vya kanisa la FPCT Mwanga na kuhitimishwa kwa tamasha kubwa katika uwanja wa Lake Tanganyika likisindikizwa na waimbaji waliopo mkoani hapo na wale waishio nje ya mkoa huo kama Victor Aron, Upendo Nkone,...
ROSE MUHANDO AKAMILISHA ALBUM MPYA CHINI YA SONY MUSIC AFRIKA YA KUSINI Malkia wa muziki wa gospel nchini bibie Rose Muhando hatimaye amemaliza kurekodi album yake mpya ya sauti pamoja na kurekodi nyimbo mbili kwenye video huko nchini Afrika ya kusini chini ya kampuni ya Sony Music Entertainment ya Afrika ya kusini. Kwa mujibu wa taarifa alizotoa mwimbaji huyo hii leo amesema amekamilisha nyimbo tatu zilizokuwa zimebakia katika kukamilisha album hiyo ya sauti ambayo hata hivyo hajaitaja jina. Mwimbaji huyo ambaye aliingia mkataba na kampuni hiyo ya kimataifa mapema mwaka jana, tayari...
WAPENZI WA MUZIKI WA GOSPEL JIJINI NAIROBI KUKUTANISHWA NA PAUL MWAI Paul Mwai mwandaaji wa tamasha hilo.                    Wapenzi wa muziki wa gospel jijini Nairobi nchini Kenya wanatarajiwa kukutanishwa pamoja siku ya tarehe 2 mwezi ujao katika uwanja wa mpira wa Thika kwenye tamasha kubwa la muziki wa injili lililoandaliwa na mwimbaji aliyejipatia umaarufu siku za karibuni Paul Mwai ambaye ameamua kulipa jina  tamasha hilo kama  Groove awards skiza tune of the year celebration. Mwimbaji huyo ambaye amefahamika zaidi...
MFALME WA R&B AFRIKA YA KUSINI AOKOKA, APOTEZA DILI YA KUFANYA KAZI NA MMAREKANI Loyiso Bala mfalme wa R&B Afrika ya kusini aliyeamua kuokoka. Mashabiki wa mwanamuziki Loyiso Bala wa Afrika ya kusini ambaye amekuwa akitamba na aina yake ya muziki R&B kwa muda mrefu, hivi karibuni walipigwa na butwaa wengine kucheka na kushindwa kuamini walichokuwa wakikisikia kutoka kwa mwimbaji huyo pale alipoamua kuwasilimia kwa salamu ya ''Nawasalimu kwa jina la Bwana na mwokozi wetu Yesu Kristo'' ikiwa katika uzinduzi wa album yake ya CD na DVD aliyoipa jina la ''Love Complete''. Mwimbaji...
KWA TAARIFA YAKO--WADOGO ZAKE UCHE WOTE WAFUATA NYAYO ZA WAZAZI ''WACHUNGAJI'' Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu cha ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu Pastor Uche akiwa na mdogo wake anayemfuatia Pastor Samuel Bruno. Ninadra sana kukuta familia...

HEBU MFAHAMU EPHRAM SEKELETI KUTOKA ZAMBIA MWIMBAJI MAALUFU WA NYIMBO ZA INJILI

HEBU MFAHAMU EPHRAM SEKELETI KUTOKA ZAMBIA MWIMBAJI MAALUFU WA NYIMBO ZA INJILI
HISTORIA YA MWANAMUZIKI WA INJILI EPHRAIM SEKELETI MUTALANGE Ephraim Sekeleti Ephraim Sekeleti Mutalange ni muimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini Zambia, alizaliwa Mwaka 1983 katika mji wa Kalulushi nchini Zambia. Alimaliza elimu yake ya sekondari katika shule ya Kalulushi mwaka 2001. Ephraim ni mtoto wa pili toka mwisho kati ya watoto sita, aliingia kwenye muziki wa injili tangu akiwa kinda huku alifundishwa kupiga kinanda na mmishonari alipokuwa bado mdogo. Mama yake anasema  “ Ephraim alikuwa ni mtoto aliyekuwa wa kelele nyingi”. Yeye pamoja na dada zake waliimba...

HIVI NDIVYO LOVE TANZANIA FESTIVAL ILIVYOKUWA KATIKA VIWANJA VYA JANGWANI

HIVI NDIVYO LOVE TANZANIA FESTIVAL ILIVYOKUWA KATIKA VIWANJA VYA JANGWANI
Maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es salaam hapo jana waliweza kufurika katika viwanja vya Jangwani jijini   hapa ili kupata baraka zao katika sherehe za Ipende Tanzania (Love Tanzania Festival) inayoongozwa na muhubiri Andrew Palau akishirikiana na waimbaji kutoka ndani na nje ya nchi wakiongozwa na Don Moen na mwanadada Nicole C. Mullen ambao wameweza kuwabariki wengi kwa huduma yao. Katika siku ya kwanza hapo jana watu walipigwa butwaa kuona mchezo wa kuruka na pikipiki, uimbaji na muziki kwa ujumla hasa wakati walipoimba waimbaji Nicole na Don Moen vyombo viliweza kusikika...

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog