Posted by Unknown
Posted on 8:49 AM
with 1 comment
 |
Marehemu Fanuel Sedekia. |
Ikiwa takribani miaka minne tangu kufariki kwa mwanamuziki mashuhuri wa
muziki wa injili nchini Fanuel Sedekia huko nchini Israeli alikokwenda
na msafara wa mwalimu Christopher Mwakasege kwa ajili ya kutembelea
maeneo matakatifu naye mama yake mzazi Eunice Sedekia amefariki dunia
usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Mount Meru jijini Arusha
alikokuwa akipatiwa matibabu.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo GK imezipata ni kwamba mama huyo amefariki
dunia usiku wa saa tatu hospitalini hapo, ambapo msiba na mipango ya
mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Fanuel Sedekia maeneo ya White
Rose jijini Arusha.
Tunaiombea familia ya Marehemu Sedekia, Mungu awatie nguvu na uvumilivu na wazidi kumtukuza Mungu kwa maana ni yeye tu mwenye mamlaka juu ya maisha yetu. amna
ReplyDelete