KWA TAARIFA YAKO--LIFAHAMU KANISA JIJINI DAR LENYE WAIMBAJI WENGI MAARUFU
KWA TAARIFA YAKO alhamisi ya leo ni kwamba kama tunavyojua kuna makanisa mengi nchini yamejaaliwa kuwa na waimbaji binafsi pamoja na vikundi vya kwaya ambavyo hutumika kumsifu Mungu katika ibada zao katika sharika hizo, ila pamoja na hayo kuna jambo hulijui ama walijua kuhusiana na kanisa la Evangelistic Assemblies of God (E.A.G.T) Mito ya baraka kwa askofu Bruno Mwakiborwa ambao wanapatikana mitaa ya kariakoo mkabala na klabu ya soka ya Yanga.
GK inaweza kuthubutu kusema kwamba kanisa hili ndio linaloongoza kwakuwa na idadi kubwa ya vikundi vya kwaya na waimbaji binafsi nchini ambao asilimia kubwa wote ni maarufu, kati ya waimbaji hao wanaopatikana katika kanisa hilo ni pamoja na Bahati Bukuku, Flora Mbasha, Boniface Mwaitege, Ambele Chapanyota, J'sisters, Lugano Mwiganege, Rhema Singers, New Jerusalem Choir, Ebenezer Choir, Sifa John, Lyanga George, Emmanuel Mgaya a.k.a Masanja Mkandamizaji na waimbaji wengine wengi ambao wanaendelea kumiminika katika kanisa hilo bila kumsahau kijana Silas Mbise ambaye ni mwalimu wa kwaya ya New Jerusalem pia mtangazaji wa Wapo Radio lakini kwwasasa nayeye ameamua kujikita kwenye muziki kama mwimbaji binafsi kwa kutanguliza single yake iitwayo Naja Bwana.
Kanisa hilo limekuwa na utaratibu wa kufanya uinjilisti sehemu mbalimbali jijini Dar es salaam kwenye mikusanyiko ya watu kama Kariakoo, Karume na sehemu nyinginezo ambapo wamekuwa wakivuta umati wa watu na wengine kumpa Yesu maisha yao kutokana na injili wanayoisikia kupitia neno la Mungu pamoja na uimbaji unaobariki wengi.
![]() |
J'sisters |
Askofu Mwakiborwa akimtambulisha Masanja katika moja ya mikutano yao ya nje ya uinjilisti. |
![]() |
Flora na mumewe Emmanuel Mbasha katika picha ya pamoja. |
Boniface Mwaitege na Bahati Bukuku wakifurahia jambo. |
Baadhi ya vijana watanashati wanaopatikana kanisa la mito ya baraka. |
Baadhi ya waimbaji wa New Jerusalem Choir watoto wa mito ya baraka katika picha ya pamoja. |
Umati ukisikiliza injili maeneo ya Karume wakati kanisa hilo lilipokuwa likifanya uinjilisti eneo hilo. |
Moja ya magari ya kanisa hilo yakiwa katika uinjilist |
0 comments:
Post a Comment