MCHUNGAJI PETER MSIGWA AENGULIWA KUWANIA UENYEKITI WA CHADEMA JIMBO LA IRINGA MJINI
![]() |
Add caption |
KUELEKEA
UCHAGUZI WA CHADEMA IRINGA MJINI: Habari zisizo rasmi kutoka eneo la chumba
cha mkutano mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) zimedai kwamba Mchungaji
Peter Msigwa ameenguliwa kutetea nafasi yake ya uenyekiti.
Ameenguliwa kwa kile kilichoelezwa na
wapashaji wetu kwamba anachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza makundi ndani ya
chama hicho.
Makundi hayo yanaelezwa kukiwekwa rehani
chama hicho wakati kikijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Pamoja na Mchungaji Msigwa, taarifa hizo
zimesema Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Chiku Abwao (Chadema) naye
ameenguliwa kuwani nafasi yoyote ya uongozi katika chama hicho mkoani hapa.
Hivikaribuni Abwao alinukuliwa akitangaza
kuwania nafasi ya uenyekiti wa mkoa wa chama hicho unaotarajia kufanyika
Jumapili keshokutwa.
Kuenguliwa kwa Msigwa katika uchaguzi huo
kumeacha kampuni wagombea wawili wanaomenyana katika nafsi hiyo itakayosaidia
kutoa picha ya jinsi mambo yatakavyokuwa wakati wa mchakato wa kumpta mgombea
ubunge jimbo la Iringa Mjini mwaka 2015.
Wagombea hao ni Frank Nyalusi anayeelezwa
kuwa ni mfuasi wa kufa na kupona wa Mchungaji Peter Msigwa na Mohamed Makuke
ambaye ni mfuasi wa kundi la wengi linalodaiwa kumpinga Mchunngaji Msigwa.
Kundi linalojiita la wengi katika chama
hicho limesikika likisema mara kwa mra kwamba tabia ya Mchungaji Msigwa ndani ya
chama hicho inawaweka katika wakati mgumu wa kutetea nafasi ya ubunge mwaka
2015.
Mchungaji Msigwa ni kiongozi
asiyeambilika, anayejua kila kitu, mbishi, kaidi, mwenye kiburi, asiyependa
watu, mwenye visasi, majivuno na asiyetaka ushirikiano toka kwa wenzake, asiye
na mikakati ya kujenga chama huku akiamini siasa za kitaifa pekee anazopenda
zaidi zinaweza kulinusuru jimbo hili katika Uchaguzi Mkuu wa mwakani.
Wakati Mchungaji Msigwa akirushiwa lawama
zote hizo, taarifa za uhakika zimedai kwamba ofisi ya wilaya ya chama hicho
imefungwa na wameamuliwa kuondoka baada ya uongozi wa mbunge huyo unaomaliza
muda wake kushindwa kulipa kodi ya pango. Mchungaji Msigwa ndiye Mwenyekiti wa
Chadema jimbo la Iringa Mjini anayemaliza muda wake hii leo.
Wanachama wa chama hicho wamechukizwa kwa
hatua ya mbunge wao kuridhia kupoteza ofisi pekee ya chama hicho mjini Iringa
kwasababu ya kushindwa kulipa Sh 540,000 walizokuwa wakidaiwa.
Matokeo ya uchaguzi huo yanatarajiwa
kutangaza baadaye hii leo.
0 comments:
Post a Comment