Home » »

AJALI YA GARI YAUA WATU 6 NA KUJERUHU VIBAYA WENGINE 18 HUKO MKOANI RUVUMA

WATU sita ambao ni abiria waliokuwa wakisafiri kwa basi kutoka Mbinga mjini kwenda makao makuu ya wilaya mpya ya Nyasa, mkoani Ruvuma wamefariki dunia na wengine 18 kujeruhiwa vibaya baada ya gari hilo walilokuwa wamepanda, kuacha njia na kutumbukia kwenye korongo.
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi, Kamanda wa Polisi wa mkoa huo Mihayo Msikhela, alisema gari hilo lenye namba za usajili T 759 BVR aina ya Nissan Civillian lilipata ajali Agosti Mosi mwaka huu, majira ya saa 10:30 jioni katika kijiji cha Burma kata ya Nyoni wilayani Mbinga.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela akimtaka hali mmoja kati ya majeruhi Joseph Matembo aliyelazwa katika hospitali ya wilaya ya Mbinga
Mihayo alifafanua kuwa ajali hiyo ilisababishwa na gari kuwa katika mwendo kasi, ambapo dereva aliyekuwa akiliendesha alishindwa kulimudu kwenye kona kali na hatimaye lilitumbukia katika shimo kubwa (korongo) na kusababisha mauaji na majeruhi hao.
“Mpaka sasa dereva aliyekuwa akiliendesha gari hili bado jina lake halifahamiki kutokana na kukimbia kusikojulikana, Jeshi la polisi tunafanya jitihada ya kumtafuta ili aweze kupatikana na baadaye tupate maelezo yakinifu juu ya tukio hili”, alisema Mihayo. 

Aliwataja walimu wa shule ya msingi waliofariki dunia kuwa ni Esther Kumburu wa shule Kilimani wilayani Mbinga na Efigenia Kayombe ambaye ni mwalimu wa shule ya Linda iliyopo Mbambabay wilayani Nyasa.
Vilevile kulikuwa na Ernest Ndunguru mkazi wa kijiji cha Mikalanga wilayani Mbinga, Anna Chitete kijiji cha Kilosa wilayani Nyasa na mmoja ambaye alifahamika kwa jina moja la Mbunda mkazi wa kitongoji cha Lusonga Mbinga mjini, na kwamba maiti moja ambaye ni wa kiume bado hajatambuliwa jina lake mpaka sasa.
Aidha Kamanda Mihayo alieleza kuwa maiti zote zimehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Mbinga, na kwamba majeruhi bado wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo lakini hali zao bado ni mbaya.
Hata hivyo alitoa wito kwa madereva wote mkoani Ruvuma, kuacha kuendesha vyombo vya moto barabarani kwa mwendo kasi, ikiwemo vile ambavyo vimekuwa vikibeba abiria kwani kufanya hivyo kuna hatarisha maisha ya watu wanaosafiri, kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Kwa uupande wake mkuuu wa wilaya ya mbinga Senyi Ngaga alipohojiwa na jamvilahabari kwa njia ya simu  kuhusina na ajali iliyotokea alieleza kuwa taarifa hiyo ameipata akiwa Jijini Dar es salaam kwa shughuli za kikazi lakini  hawezi kuongea chochote kwa sababu yupo nje ya wailaya hiyo.
“Mwandishi labda umtafute kaimu mkuu wa wilaya ambaye nimemwachia wilaya hiyo kwani yeye ndiye atakuwa na maelezo mengi ya wilaya hiyo ila sasa hivyo yupo mbeya kwenye mkutanao wa wawekezaji alisema Senyi”
Hata hivyo kaimu mkuu wa wilaya hiyo ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya songea Joseph Joseph Mkirikiti alipohojiwa na jamvilahabari kwa njia ya simu alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo alidai kuwa  imetokea katika kijiji cha Burma kwenye eneo la mlima chunya ambapo gari hilo lilikuwa linatoka Mbinga kwenda Mbambabay.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Search This Blog