Home » »

BREEEEKING....!! MAJAMBAZI WATATU WAUAWA NA POLISI KWA RISASI WILAYANI KAHAMA....!!

Mmoja wa Majambazi hao walioko katika hospitali ya wilaya ya Kahama

Jeshi la polisi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga limefanikiwa kuwaua watu  watatu  wanaodhaniwa kuwa ni Majambazi ambao majina yao hayajafahamika waliokuwa wakipanga kuvamia mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu uliopo wilayani Kahama usiku wa kuamkia leo.
Miili ya Majamzazi hao watatu waliwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya wilaya ya Kahama
Kamanda wa polisi Mkoani humo Evarist Mangala amesema tukio hilo limetokea majira ya saa sita usiku wa kuamkia leo katika kijiji Namba Tisa, baada ya kutokea majibizano ya risasi baina ya matuhumiwa hao na Askari wa Doria.
Mangala amesema watuhumiwa hao wanaokisiwa kuwa na umri kati ya miaka 25-30, wamekutwa wakipanga kufanya uhalifu katika mgodi huo, kabla ya kuanza  kurushiana risasi na Askari Polisi na hatimaye kuzidiwa nguvu na kuuawa.
Amesema  awali jeshi la polisi lilipata taarifa kuhusu uhalifu unaotaka kufanyika katika mgodi huo, na ndipo likafuatilia na kukuta watuhumiwa hao wakiwa na mabomu matatu ya kurusha kwa mkono  wakijiandaa kufanya uhalifu katika eneo hilo.
Mangala ameongeza kuwa mbali na kukutwa na mabomu hayo ya kivita pia wamekutwa na bunduki mbili za kivita aina ya SMG zenye namba za usajili 1972PX7482 na UC-17751998 pamoja na risasi 94 ndani ya magazine nne.
Kamanda Mangala amesema miili ya Majambazi hao imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Kahama.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog