KANISA LA BETHEL PENTECOSTE BUZA NALO LAPATA KISANGA CHA MOTO
Huko Buza njia panda ya kuelekea Kitunda jijini Dar es salaam, watu wasiofahamika wamelichoma moto upande mmoja kanisa la Bethel Pentecoste linaloongozwa na mchungaji Emanuel Kapama majira ya usiku wakati waumini wakiwa tayari majumbani mwao.
Kwa mujibu wa mchungaji Kapama amesema jana walikuwa na ibada kuanzia majira ya saa 1 usiku hadi saa 2 kisha kutawanyika lakini waliporejea asubuhi wakashangaa kukuta kanisa lao limechomwa moto upande mmoja na kukuta chupa ya mafuta ya taa ambayo imechukuliwa na jeshi la polisi kwa ushahidi ikiwa ndani ya kanisa hilo huku watu hao wakiwa wameshamwaga mafuta ya taa kanisa zima ambalo limezungushiwa kwa mabati pamoja na mifuko migumu aina ya viroba.
Ambapo kwa mujibu wa mchungaji huyo amesema jeshi la polisi tayari limefika na kuangalia kilichotokea na kuchukua vitu ambavyo vitatumika kwa ushahidi ikiwemo chupa hiyo ya mafuta ya taa.
Moja ya kanisa lililochomwa moto huko mkoani Kigoma wiki hii. picha by Fungo Omary. |
0 comments:
Post a Comment