MWALIMU ALIYEISHI NA NDOO ZA KINYESI NDANI, ATOA SIMULIZI YA AJABU... USHIRIKINA WATAJWA.


Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kibasila jijini  Dar, Gaudensia Albert.

HII ni simulizi ya aibu! Tukio la mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kibasila jijini  Dar, Gaudensia Albert, mkazi wa Kisiwani Kata ya Sandali wilayani Temeke kuishi na vinyesi, mikojo na matapishi chumbani kwake, limeibua mshtuko na aibu ndani yake.
Kinyesi kikiwa kwenye ndoo.
Kwa mujibu wa mwenye nyumba, Reuben Shayo, mwalimu huyo anayefundisha masomo ya sayansi aligundulika hivi karibuni kuwa anaishi ndani ya chumba chenye rundo la uchafu huo.
Shayo alifunguka: “Siku ya tukio (Februari 22, mwaka huu) tuliona funza wakitoka chini ya mlango wa ticha na harufu mbaya.
“Ukweli ni kwamba mwenzetu hatujawahi kumuona akioga wala akiingia chooni, ndiyo tukabaini uchafu huo baada ya kuchungulia ndani.
“Yaani hakuwahi kuleta mgeni wa aina yeyote na kumwingiza ndani hivyo inaonesha dhahiri alikuwa akiogopa kuonesha uchafu wake.”
Umati wa watu waliokusanyika katika eneo la tukio.
Baada ya kugundulika kuwepo kwa uchafu huo, Shayo na wakazi hao walitoa taarifa polisi ambapo awali, Sajenti wa Jeshi la Polisi, Ramadhan Kagolo, aliwajibika kusimamia kuvunjwa kufuli la chumba hicho kwa vile kazi iliyokuwa ikifanyika ilikuwa ni kwa ajili ya kulinda afya ya jamii.
Jumatano iliyopita, Manispaa ya Temeke ilichukua uamuzi wa kuteketeza kinyesi kilichokutwa katika chumba cha mwalimu huyo baada ya maofisa wa afya wa manispaa hiyo kutaka kunusuru afya za wakazi wa eneo hilo.
Wakitoa kinyesi hicho nje.
Kazi hiyo ilifanyika majira ya saa 9:00 alasiri chini ya uangalizi wa jeshi la polisi kwa kushirikiana na mwenyekiti wa mtaa huo, Yahya Bwanga.
Wakati wa tukio hilo, Ofisa Afya wa Manispaa ya Temeke, Floyd Tembo alisema baada ya kupata taarifa za kuwepo kwa tukio hilo la kushangaza, waliwatuma watendaji wa afya wa kata hiyo wafanye utafiti wa kujua tatizo lina ukubwa gani.
“Baada ya kufanya utafiti wao pia walimpata mhusika ambapo tulichukua jukumu la kwenda kumhoji mkuu wa shule hiyo ili kujua kama mwalimu Gaudensia alikuwa na akili timamu au la.
“Hata hivyo, mkuu huyo wa shule alitueleza kuwa ana akili timamu na kwamba tukio hilo limewashtua walimu wenzake,” alisema Tembo.  
Alisema pamoja na kuuteketeza mrundikano huo wa kinyesi, bado wanaendelea na utaratibu wa kumfikisha mwalimu huyo kwenye vyombo vya sheria ili kujua kwa nini alifanya hivyo.
“Hili tukio halihusiani na ugonjwa wa akili inawezekana kuna tatizo lingine au labda mambo ya ushirikina, haiwezekani ajisaidie na kuhifadhi uchafu ndani kwake,” alisema.
Alisema mwalimu huyo hakuweza kufika kwenye eneo la tukio hali iliyofanya mlango wa chumba chake uvunjwe chini ya uangalizi wa polisi.
Tembo alisema mwalimu huyo alishindwa kutokea kwenye eneo la tukio kwa vile alipelekwa Hospitali ya Temeke kisha kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kupimwa afya baada ya kupata mshtuko ambao umesababishwa na taarifa hizo.
Afisa Afya wa Usafi wa Mazingira wa Temeke, Jumanne Muhogo alisema uchafu walioubaini ulikuwa ni uchafu wa kinyesi, mkojo na matapishi inasemekana kuna kipindi alikuwa anatapika.
“Tukio hili kwa Manispaa ya Temeke ni la kwanza kutokea, inaelekea huyu mtu hana akili ya kawaida kama angekuwa na akili ya kawaida asingeweza kufanya namna hii,” alisema.

BREAKING NEWS..!! KAPTENI JOHN KOMBA AFARIKI DUNIA.



Habari zilizotufikia muda mfupi uliopita zinasema kwamba Mbunge wa Mbinga Magharibi (CCM), Kapteni mstaafu John Damian Komba amefariki dunia.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, Kapteni Komba amefariki katika Hospitali ya TMJ, Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu kutokana na maradhi ya sukari yaliyokuwa yakimsumbua.

Komba ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tanzania One Theatre (TOT) atakumbukwa sana kwa umahiri wa utunzi wa nyimbo mbalimbali za kwaya akiwa na TOT.



Miaka mitatu iliyopita, Komba alipelekwa nchini India alikokwenda kufanyiwa upasuaji kwenye nyonga, tatizo lililomsumbua kwa muda mrefu likichagizwa na ule unene aliokuwa nao.

Upasuaji huo ulilazimika kufanyika kwenye Hospitali ya Apollo kutokana na Hospitali ya Muhimbili kuathiriwa na mgomo wa madaktari wakati huo.


Alipofika India, madaktari walisita kumfanyia upasuaji kutokana na kuwa na mwili mkubwa hivyo wakamwambia kuwa asilimia za kuamka katika upasuaji huo ni ndogo lakini Komba akawasisitiza wamfanyie tu.


Tangu wakati huo, Komba alikuwa na kibarua kikubwa cha kupunguza uzito kwani awali alikuwa na kilo 138, lakini akajitahidi kupunguza hadi kufikia kilo 128 ambazo pia aliendelea kupunguza hadi kilo 100.

Mungu ailaze roho ya Marehemu John Komba mahali pema peponi, Amen.

Kwa taarifa zaidi endelea kuperuz

Ziko hapa kurasa za mwanzo na mwisho za Magazeti ya leo February 28, 2015

.
.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
DSC00018
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Mwanaume wa Miaka 45 Ahukumiwa kifungo cha maisha Jela kwa kosa la Kumbaka Mtoto wa Miaka Minne


Mwanaume mmoja Yusufu Chatambala (45) mkazi wa Kijiji cha Makutupa Kata ya Lupeta Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma, amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kukiri kosa la kumbaka mtoto mdogo mwenye umri wa miaka minne.
 
Mwendesha mashtaka wa polisi Godwill Ikema ameiambia mahakama ya Wilaya ya Mpwapwa kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Feb 20 mwaka huu majira ya saa 12 jioni katika kijiji cha Makutupa kilichopo Wilayani Mpwapwa ambapo alimbaka mtoto mdogo wa kike mwenye umri wa miaka minne (jina limehifadhiwa).
 
Mwendesha mashtaka huyo amesema kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume cha sheria za nchi chini ya Kifungu namba 130 (1) 2 (a) na 131 (1) cha Kanuni ya Adhabu kama kilivyofanyiwa mapitio mwaka 2002.
 
Amesema kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo baada ya kumkamata alipokuwa akicheza na watoto wenzake jirani na nyumbani kwao kisha kumpeleka kwenye shamba la mahindi kisha kumbaka mtoto huyo na kusababishia majeraha na maumivu makali.
 
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpwapwa Paschal Mayumba alimtia hatiani mtuhumiwa huyo jana baada ya kukiri kutenda kosa hilo.
 
Akisoma hukumu hiyo, hakimu Mayumba amesema Mahakama inamhukumu kwenda jela kifungo cha maisha kwa kosa la kubaka mtoto ili iwe fundisho kwake na kwa wengine wanaotenda makosa kama hayo.

WATU WATATU WAFARIKI DUNIA KWA KUTEKETEA KWA MOTO KWENYE GARI.




Watu watatu wamefariki dunia kwa kuungua moto hadi kuteketea kabisa akiwemo dereva na utingo wake baada ya lori la mafuta kuacha njia na kupinduka na kuungua moto katika eneo la Maseyu barabara ya Morogoro Dar es Salaam.
 
Kikosi cha zimamoto walichukua muda kuuzima moto huo kutokana na kusambaa ambapo hata hivyo hakukua na matukio ya watu kujitokeza kuiba mafuta kama ilivyozoeleka.

Baada ya kumaliza kuuzima moto huo kikosi cha zimamoto na uokoaji wakafanya juhudi nyingine za kuvuta kwa craine na kukata kwa kutumia mashoka mabaki ya lori hilo baada ya walioshuhudia tukio hilo kueleza kuwa watu wote waliokuwemo katika gari hawakutoka ambapo baada ya muda miili mitatu iliokolewa ikiwa imeungua kabisa.


Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wakiwemo madereva wa malori ambapo walikuwa wakisafirisha mafuta katika kampuni moja Farhan Yusufu amesema lori hilo lilikua limesheheni mafuta ya Dezel mali ya kampuni ya Petrol Africa ilikua ikitokea Dar es salaam kwenda jijini Mwanza ambapo ilipoteza uelekeo na kupinduka kisha kuwaka moto.
Waliofariki dunia ni Ahmed Dilie dereva na utingo wake aliyefahamika kwa majina ya Emela na mtu mmoja ambaye bado hajaweza kufahamika mara moja.

ZITTO KABWE KUTANGAZA MAAMUZI MAGUMU YA KUJITOA CHADEMA.



MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, amesema hatma yake kisiasa ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) itajulikana katika kipindi cha mwezi mmoja kutoka sasa.
Raia Mwema linafahamu kwamba tangazo hilo la kisiasa linahusu mustakabali wake wa kisiasa ndani ya Chadema, chama ambacho amekitumikia katika maisha yake yote ya kisiasa tangu akiwa mtoto wa umri wa miaka 16.
Katika mahojiano aliyofanya kwa njia ya mtandao na gazeti maarufu la Guardian la Uingereza wiki iliyopita, Zitto alisema kuna kitu kikubwa atakifanya mwishoni mwa mwezi Machi huu.
“Sijawahi kufanya kampeni yoyote kubwa ya kisiasa kupitia mtandao wa twitter katika maisha yangu ya kisiasa, lakini nataraji kuwa nitafanya hivyo katika muda wa mwezi mmoja kutoka sasa. Fuatilieni tu twitter na mtaona,” alisema Zitto pasipo kwenda kwa undani.

Gazeti hilo la Uingereza limeanzisha utaratibu mpya wa kuhoji watu maarufu kwa kutumia mtandao wa twitter (twit interview) na Zitto alikuwa mwanasiasa wa kwanza kuhojiwa baada ya kubainika kuwa ndiye anayeongoza kwa kuwa na wafuasi wengi kwenye mtandao huo hapa nchini.
Akizungumza na gazeti hili kuhusu nini hasa anataraji kukifanya mwishoni mwa mwezi Machi kama alivyozungumza na gazeti hilo, Zitto alisema ni mapema kwa sasa kuweka kila kitu hadharani lakini wakati ukifika kila kitu kitakuwa wazi.
“Niseme kwamba kwenye mahojiano yale nilisema hivyo kweli na nakuhakikishia kuwa kuna tukio litatokea mwishoni mwa mwezi Machi. Ni tukio gani na linahusu nini bado mapema kusema.
“Ila naomba kuahidi Watanzania kuwa watafahamu kila kitu kuhusu tukio hilo wakati ukifika. Hiyo kampeni ambayo itaendeshwa kupitia mtandao wa twitter na mingineyo, itakuwa ya kisasa na ya uhakika kuliko yoyote ambayo imewahi kuendeshwa katika historia ya Tanzania, “ alisema.
Zitto alikataa kusema lolote kama tangazo hilo litahusiana moja kwa moja na kuhama kwake kutoka Chadema kwenda ACT au chama chochote kingine cha siasa hapa nchini zaidi ya kusema; “subirini”.
Kwa sasa, Zitto ni Mbunge na mwanachama wa Chadema kwa sababu tu ya zuio ambalo Mahakama Kuu kupitia Jaji John Utamwa liliweka katikati ya mwaka jana la kufukuzwa kwake ndani ya chama hicho kutokana na kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho.
Zitto na wenzake, Profesa Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba, walifukuzwa na Chadema kwa madai ya kupanga mapinduzi ya kumng’oa madarakani Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.
Mwigamba na Kitila wamehamia katika chama kipya cha siasa cha ACT; Mwigamba akiwa Katibu Mkuu wa muda na mwenzake mshauri na Zitto mwenyewe amekuwa akihusishwa na chama hicho.
Akizungumzia mahojiano hayo ya Zitto na Guardian, Dk. Kitila Mkumbo alisema aliyasoma mahojiano hayo lakini akasema anayejua nini kitatokea mwishoni mwa Machi ni Zitto mwenyewe.
“Mimi kama mshauri wa ACT nasema Zitto kama mwanasiasa makini ana mawazo yake na mipango yake. Mimi nasisitiza tu kwamba kama ataamua kuja ACT basi tunamkaribisha kwa mikono yote miwili.
“Tunaamini kwamba yeye ni muumini wa dhana ya Unyerere (Nyerereism) ambayo ndiyo msingi mkuu wa sera za ACT. Kama ataamua vinginevyo, sisi pia tutamuunga mkono kwa sababu tunajua itakuwa kwa nia njema,” alisema.
Katika mahojiano hayo na Guardian, Zitto aliulizwa kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu siasa na Tanzania, ikiwamo changamoto za kisiasa, hifadhi za jamii na nguvu ya mitandao ya kijamii katika siasa za hapa nchini.
Zitto alisema silaha kubwa ya maendeleo ambayo Tanzania inayo kwa sasa ni wingi wa vijana ambao alisema kama watawekewa mipango mizuri na kuwezeshwa kutumika kwa kadri ya uwezo wao, Taifa litapiga hatua kubwa.
Alisema fursa hiyo ina hatari yake nyingine kwamba chini ya asilimia 20 ya Watanzania hawana ulinzi wowote wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii, jambo alilosema ni hatari kwa mustakabali wa Taifa.
Alisema pia kwamba kwa sasa Watanzania wengi wana ufahamu wa masuala ya mitandao ya kijamii, lakini akasema idadi ya wanaoitumia ni ndogo; huku akibainisha kuwa baadhi ya viongozi wa juu wa serikali hawako hata kwenye mitandao kama twitter.
Zitto ana wafuasi zaidi ya 200,000 katika mtandao wa twitter akiwa anaongoza kwa wafuasi; huku katika nchi nyingine barani Afrika wanaoongoza wakiwa marais, wanamichezo na wanamuziki maarufu kama Didier Drogba wa Ivory Coast na Wiz Kid wa Nigeria.

Andrew Chenge AGOMA Tena Kuhojiwa na Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma.....Aomba Aruhusiwe kukata Rufaa Mahakama kuu.


MBUNGE wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge ameendelea kupambana ili Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma, lisiendelee kusikiliza shauri lake, licha ya pingamizi lake kutupiliwa mbali jana.
 
Chenge amewasilisha ombi la kukata rufaa Mahakama Kuu dhidi ya uamuzi wa baraza hilo, uliotolewa jana na kusomwa na Jaji Hamisi Msumi, ukisema madai yaliyowasilishwa kwenye pingamizi la mbunge huyo, hayalihusu baraza hivyo shauri linapaswa kuendelea kusikilizwa kama ilivyopangwa.
 
“Tumeliangalia kwa makini pingamizi hili (la Chenge) na kuipitia amri ya Mahakama Kuu inayozuia suala la akaunti ya Escrow kujadiliwa na tumejiridhisha kuwa, Baraza hili halihusiani na orodha ya watu waliotajwa kwenye amri hiyo waliyowekewa pingamizi,” alisema Jaji Msumi.
 
Alisema baraza hilo limebaini katika amri hiyo, yako makundi yaliyotajwa kutojihusisha na suala hilo hadi pale Mahakama Kuu itakapotoa uamuzi katika kesi ya msingi na katika makundi hayo, Baraza hilo la Maadili halikutajwa.
 
Alisema pia pingamizi kubwa, lililowekwa katika amri hiyo ni kuzuia kupelekwa bungeni na kujadiliwa kwa taarifa ya ukaguzi maalumu wa miamala ya Escrow na masuala ya umiliki wa IPTL.
 
“Hivyo basi, Baraza limeona hoja iliyowasilishwa na kukabidhiwa na mlalamikiwa haina msingi, hivyo imekataliwa,” alisema Jaji Msumi.
 
Chenge ang’ang’ana Baada ya uamuzi huo, Chenge aliomba kuwasilisha hoja yake ya kukata rufaa akisema, “sina nia ya kubishana, ila nataka kuwasilisha nia ya kukata rufaa kwenda Mahakama Kuu, kupinga uamuzi huu wa Baraza ili suala hili litolewe uamuzi upya”.
 
Alisema anashangazwa na wanasheria wa baraza hilo, ambao hawajatumia muda wao ipasavyo kwa kwenda masjala ya Mahakama Kuu na kupitia amri hiyo ya Mahakama Kuu na kujiridhisha, kwa kuwa amri hiyo iko wazi, pana na imegusa maeneo mengi kuliko inavyofikiriwa.
 
“Naomba nitumie haki yangu ya kukata rufaa na kwenda Mahakama Kuu, naomba nipatiwe mwenendo mzima wa kesi, sasa sijui Baraza hili lina utaratibu wa kukata rufaa au mimi ndio nitalitambulisha suala hili kwa mara ya kwanza,” alihoji Chenge.
 
Kwa upande wake, Jaji Msumi alisema baraza hilo limemruhusu mbunge huyo ambaye pia aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akate rufaa dhidi ya uamuzi wa baraza hilo Mahakama Kuu, jambo litakalosaidia pia kuweka historia ya kisheria.
 
“Ni vyema tuachie Mahakama Kuu ambacho ni chombo cha juu kuliko Baraza hili, ili itueleze kama ni sahihi sisi kuendelea na shauri hili au la, kwa sasa sina uhakika kama kanuni zimetengwa kuhusu masuala ya rufaa kwenye Baraza hili,” alisema.
 
Alisema endapo Mahakama Kuu itaamua baraza hilo lisiendelee kusikiliza shauri hilo, shauri hilo halitasikilizwa, lakini ikiamuru liendelee, litaendelea kumhoji Chenge na kesi yake ya kukiuka maadili ya uongozi wa umma.
 
Juzi Chenge alisomewa rasmi mashitaka yanayomkabili na Mwanasheria wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Hassan Mayunga, ambayo ni pamoja na kutumia madaraka yake vibaya alipokuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kushauri Serikali iingie mkataba wa miaka 20 na kampuni ya IPTL.
 
Aidha, anadaiwa baada ya kustaafu wadhifa huo wa uanasheria mkuu wa Serikali Desemba 24, mwaka 2005, mwaka 2006 aliingia mkataba wa kuwa mshauri mwelekezi wa kampuni wa VIP Engineering and Marketing Limited iliyokuwa na hisa za asilimia 30 kwenye kampuni ya IPTL.
 
Lakini, pia mwanasheria huyo anadaiwa na baraza hilo, kuingia mkataba na kampuni ya VIP, uliompatia manufaa ya kifedha ya Sh bilioni 1.6 kinyume na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma na fedha hizo ziliingizwa Februari 5, mwaka jana katika akaunti ya mlalamikiwa namba 00120102523901, iliyopo kwenye Benki ya Mkombozi Tawi la St Joseph jijini Dar es Salaam.
 
Baada ya kusomewa mashitaka hayo juzi, mbunge huyo alikataa kesi hiyo kusikilizwa na kuwasilisha pingamizi hilo la kutaka suala hilo kutoendelea kusikilizwa kwa kuwa tayari kuna kesi ya msingi Mahakama Kuu inayoendelea kusikilizwa.

Mwanamke Auawa na Mumewe Kwa Kipigo na kisha Mwili wake Kufukiwa katika Zizi la Ng'ombe


Mwanamke mmoja mkazi wa Kijiji cha Ubetu Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, amefariki dunia baada ya kupigwa na mume wake sehemu mbalimbali za mwili na kisha kuzika mwili wake kwenye boma la ng'ombe.
 
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Geofrey Kamwela, alisema tukio hilo lilitokea Februari 25 mwaka huu saa 11:45 jioni.
 
Akieleza mazingira ya tukio hilo, Kamanda Kamwela, alisema siku ya tukio jirani na familia hiyo alipigiwa simu na mume wa marehemu na kumwambia ameuwa mkewe na kumtelekeza ndani ya bomala ng’ombe.
 
Kwa mujibu wa kamanda, mwanamke huyo aliyeuawa ametajwa kuwa ni Jenipher Peter (45). Alisema alikuwa akiishi na mume wake, Peter Mrosso (43) pamoja na watoto wao watatu. Alisema mwili wake ulifukiwa ndani ya boma la ng'ombe.
 
Kamanda alisema taarifa za mauaji ya mwanamke huyo ilitolewa baada ya jirani yake kupigiwa simu na mume wa marehemu, akimtaarifu kuwa amemuua mkewe na maiti ameifukia ndani ya boma la mifugo.

Wafuasi wa CUF Wawazidi Ujanja Polisi Mahakamani.....Kesi yapigwa kalenda hadi March 23


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam,jana iligeuka mithili ya uwanja wa sinema baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) kuwafutia mashitaka watu 30 wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF) kutimua mbio na kutoweka eneo la mahakama hiyo.

Kitendo hicho kiliwafanya wafuasi hao wanusurike kuunganishwa katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, katika mahakama hiyo.

Tukio hilo lilitokea jana saa 5:00 asubuhi baada ya upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka, Mawakili wa Serikali, Joseph Maugo na Mwanaamina Kombakono, kudai kuwa DPP amewasilisha hati ya kuwafutia kesi washtakiwa na hivyo, hana nia ya kuendelea kuwashitaki.
Alidai DPP analiondoa shauri hilo chini ya kifungu cha 91 (1) cha Mwenendo wa Sheria za Makosa ya Jinai (CPA).

Hakimu Mchauru alisema kwa kuwa DPP ameona hana nia ya kuendelea kuwashitaki, mahakama yake haina sababu ya kuendeleaa kuwashikilia washtakiwa, hivyo inawaachia huru.

Baada ya washtakiwa hao kuachiwa huru walitoka eneo la mahakama na kutimua mbio wakiwa sambamba na wadhamini wao.

Saa 5:10 asubuhi, mahakama hiyo iliyoketi chini ya Hakimu Mchauru, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Lipumba alipanda kizimbani kusikiliza kesi yake.

Jopo la mawakili wa serikali liliomba mahakama kubadilisha hati ya mashitaka na kuwaunganisha wafuasi 30 pamoja na Profesa Lipumba, wakati huo wakiwa wamekwishaondoka katika eneo la mahakama na kutawanyika.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 23, itakapotajwa tena wakati washtakiwa wote wakiwa nje kwa dhamana.

JWTZ Watoa Tamko Baada ya Ajali ya Ndege ya Kivita Iliyotokea Mkoani Mwanza Leo


Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa ya ajali ya Ndegevita moja (1) iliyotokea leo tarehe 27 Februari 2015 katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Mwanza.

Ndegevita za JWTZ zilikuwa katika mazoezi ya kawaida ya kivita, Wakati rubani wa ndegevita iliyopata ajali akijiandaa kuruka ndipo ndege mnyama akaingia katika moja ya injini zake na kusababisha ndegevita kuwaka moto.

Hata hivyo, rubani wa ndegevita hiyo Meja Peter Lyamunda alipoona ndege yake inawaka moto alifanikiwa kujirusha nje ya ndege hiyo kwa kutumia vifaa maalum na kufanikiwa kuokoa maisha yake ingawa amepata majeraha katika mguu wakati wa kujiokoa. Kwa sasa hali yake ni nzuri anaendelea na matibabu ya kawaida .

Wananchi wasiwe na hofu hii ni ajali ya kawaida , waendelee na shughuli kama kawaida na kwamba sehemu ilipoangukia haikuleta madhara yoyote ya binadamu, nyumba wala miundo mbinu. 

Baadhi ya Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa eneo la tukio kuangalia mabaki ya ndegevita hiyo iliyopata ajali leo.

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog