Home » » Duniani Uingereza walivyoamua kujenga maeneo ya kuvutia ‘unga’.. ndio kusema wamehalalisha?

Duniani Uingereza walivyoamua kujenga maeneo ya kuvutia ‘unga’.. ndio kusema wamehalalisha?

Mapambano ya dawa za kulevya yako kila kona duniani… najua kukutana na kichwa cha habari kwamba kuna nchi eti wameamua kuwajengea kabisa vibanda vya kuvutia dawa za kulevya ni kitu ambacho kinaweza kukushtua, lakini habari iko hivyo !!
Kuna ripoti za watu wenye majina makubwa duniani kuripotiwa kufariki kwa kuzidisha dawa za kulevya… hizo ripoti zipo pia zinazowahusu watu wa kawaida ambao ni watumiaji wa dawa hizo… Ireland wameenda mbali kidogo kwa kuamua kuwaokoa watu hao.
Kinachofanyika ni kulegeza kidogo sheria za Ireland, wako kwenye mpango wa kuanzisha vituo vya kuvutia dawa za kulevya… kingine  ni kwamba kwa sasa mpango wao mwingine ni kuhakikisha wanaruhusu watumiaji kuwa na kiasi kidogo cha heroin, cocaine na bangi kwa ajili ya matumizi ya mtumiaji binafsi.
Daktari mmoja amesema kuna wastani wa mtu mmoja kufariki kila siku kwa kujizidishia dawa za kulevya Ireland, lakini duniani kuna maeneo 90 yaliyowekwa maalum kwa watumiaji wa dawa za kulevya na haijawahi kutokea mtu akafariki.
Kwenye utetezi wa uamuzi wao, Ireland wamesema kwenye vibanda hivyo kutakuwa na usimamizi mzuri utakaofanya wanaojidunga wasizidishe kiwango cha dozi ya dawa na kutokea matatizo mengine.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog