Home » »

hata kama;;;

lion
MAPENZI YA KWELI
Mapenzi ya kweli

Kwenye nyumba tunazoishi mara nyingi tumekua tukifuga na kuishi na Paka au Mbwa kitu ambacho ni kawaida na ni nadra sana kukutana na mtu anaeishi na au kufuga viumbe ambavyo ni hatari kwa maisha ya binadamu mfano Nyoka.
Sasa hii inaweza kutushangaza kwa sababu kuna Simba ajulikanaye kama mkuu wa msitu alihamishia makazi yake kwenye nyumba ya Melanie Griffith mwigizaji ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 57.
Unaambiwa Simba huyu alihamia kwenye nyumba hiyo toka Melanie akiwa na umri wa miaka 14 huko Sherman Oaks,California Marekani ambapo mama yake Melanie ni mwigizaji Tippi Hedren na baba yake wa kambo kwa muda huo Noel Marshall.
Kingine cha kufahamu ni kwamba hii familia ilikuwa inamlea Simba huyu nyumbani ambae alipewa jina la Neil kama wanyama wengine, mfano Mbwa au Paka.
Picha za Melanie na mama yake wakiwa wanacheza na simba huyo ziliwekwa kwenye jarida la ‘Life Magazine‘ mwaka 1971 ambapo zilikua zinaonesha mtoto huyo kuwa na ukaribu mkubwa na Simba na hata kulala na kuogelea nae.
Mama Melanie aliyeigiza kwenye filamu ya ‘The Birds’ miaka 8 baada ya kupigwa kwa picha hizo alionekana pia kupenda kucheza na mnyama huyo pori.
Simba huyu alikuja kuishi na familia hiyo wakati mama Melanie na baba wakiwa wanatengeneza filamu Afrika ambapo kwenye matembezi yao waliona kuna nyumba yenye Simba ambao hawana makazi mazuri ndipo walipoamua kumchukua Simba huyo kutengeneza filamu inayohusiana na Simba.
Kweli baadae walitengeza filamu iliyoitwa ‘Roar’ ambapo ilitolewa kwenye miaka ya 80 ambapo kwenye mahojiano yaliyofanywa mwezi April mwaka 1982 na The Guardian, U.K ilitangazwa filamu hiyo ya Roar.
Griffith alielezea jinsi alivyopata alama za usoni na kusema Simba huyo hakumaanisha kumuumiza, aliendelea kusema ‘Baada ya kukaa miaka 7 na Simba unasahau kama Simba ni mnyama na pia ni hatari kuwa nao karibu, katika utengenezaji wa filamu hamna mnyama alieumia sema watengenezaji wengi wameumia na wapo hospitali’
Mama wa Griffith ambaye sasa ana miaka 85 alipendezwa sana na uhusiano wa Griffith na wanyama mpaka akaamua afungue kituo cha kulea wanyama ambao wamekosa malezi kiitwacho ‘Shambala Preserve’ kwenye mjia wa  Acton California Marekani mwaka 1972.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog