Home » »

BARCLAY'S IRINGA YAWAFUNDISHA WANAFUNZI WA IRINGA MBINU ZA UTUNZAJI WA FEDHA

Meneja wa Barclays tawi la Iringa Shamsa Abdul-Latif wakati wa mafunzo hayo
Akifafanua namna wanafunzi wanavyoweza kujiwekea akiba kwa kuzingatia mahitaji yao ya msingi
Wakati mada zikiwasilishwa
Maafisa wa benki hiyo katika picha
Mshauri wa Huduma kwa Wateja wa benki hiyo, Julius Ngwilla
Afisa Mikopo, Charles Mwakameta alipokuwa akifafanua njia mbalimbali za kutunza fedha
Wakati wa Majadiliano ya vikundi
Katika majadiliano ya vikundi
Na baada ya mafunzo hayo msosi ukapigwa. Walianza wanafunzi
Wakaja maafisa wa Barclays
Wakaendelea maafisa hao
BENKI ya Barclays tawi la Iringa imetoa mafunzo ya utunzaji wa fedha kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Highlands ya mjini hapa waliokiri matumizi ya pombe yanazifanya baadhi ya familia zao kukosa akiba.

Katika majadiliano yao, wanafunzi hao walitaja vipaumbele vya familia zao kwamba ni malazi, chakula, maji, shule na mavazi hata hivyo wakasema pamoja na umuhimu wake, matumizi ya pombe na vitu vingine vya anasa yanadhohofisha upatikanaji wa huduma hizo kwasababu ya kukosa akbia.  

Meneja wa tawi hilo, Shamsa Abdul Latiff alisema katika mafunzo hayo yanayotarajiwa kuwanufaisha wanafunzi wa shule nyingine za mkoani hapa kwamba, kila mtu anaweza kufikia ndoto ya mahitaji yake kama atakuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha.

Aliyataja mahitaji hayo kuwa ni pamoja na kumudu gharama za elimu, ujenzi, ununuzi wa vyombo mbalimbali vya usafiri, vyakula na huduma nyingine muhimu kwa matumizi ya binadamu.

“Wanafunzi mnaweza kujiwekea akiba kutokana na kidogo mnachopewa na wazazi wenu kwa ajili ya matumizi yenu ya kila siku muwapo shuleni, lakini pia mnaweza kusaidia kuwashauri wazazi na walezi wenu kujiepusha na matumizi yasio ya lazima ili mpate akiba,” alisema.

Meneja huyo alitoa mfano akisema katika kila Sh1,000 anayopewa mwanafunzi kwa ajili ya matumizi yake shuleni anaweza kujiwekea akiba ya hadi nusu ya kiasi hicho ambacho kwa mwaka kinaweza kuwa kikubwa.

“Ukimudu kuweka akiba, kwa mfano ya Sh 500 kila siku, mwisho wa mwezi utakuwa na Sh 15,000 na mwisho wa mwaka utakuwa na zaidi ya Sh 180,000 na kwa miaka sita ya elimu ya sekondari utakuwa na zaidi ya Sh Milioni moja unayoweza kuitumia kwa mambo mengine ya kimaendeleo,” alisema.

Latiff alisema zipo njia ya nyingi za kuhifadhi akiba ya fedha na akaitaja iliyo ya uhakika na usalama zaidi kuwa ni kwa kupitia benki.

Awali Afisa Mikopo na Ufunguzi wa Akaunti wa benki hiyo, Charles Mwakameta alizitaja njia nyingine za kutunza fedha kuwa ni pamoja na kuficha sehemu mbalimbali majumbani kama kwenye mito na vitandani.

Zingine ni pamoja na kuhifadhi kwa kununua bidhaa mbalimbali kama vyakula kwa lengo la kuziuza pale unapohitaji fedha, kwa marafiki, kwenye makampuni ya simu, vikundi vya upatu na vyama vya kuweka na kukopa.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog