Home » »


ASKOFU DR SOLLO AMSHAURI RAIS KIKWETE KULIVUNJA BUNGE LA KATIBA, AWASHANGAA UKAWA KWA VURUGU

Rais Dr Jakaya Kikwete
Viuongozi  wa UKAWA

   Askofu Dr Boaz Sollo akiwa katika moja kati ya mikutano  yake ya  kuliombea Taifa amani 



UMOJA  wa  katiba ya  wananchi (UKAWA)  wazidi  kukaliwa kooni baada yaaskofu  wa  kanisa la Overcomers Power Centre Iringa Dr  Boaz Sollo kupinga vikali uamuzi  wa UKAWA kutoka bungeni na kwenda kwa wananchi kabla ya kuifanya kazi  waliyotumwa  bungeni kama  wajumbe wa  bunge la katiba na  hivyo  kumshauri  Rais wa jamuhuri ya muungano  wa Tanzania Dr Jakaya Kikwete kulivunja bunge  hilo ili kuepusha amani kuvurugwa  nchini.

Huku akisema kuwa akiwa kama mtumishi  wa Mungu anaamini kabisa kuwa  serikali mbili ni jibu la watanzania  katika  endeleza umoja ,amani na mshikamano ulioachwa na waasisi  wa Taifa  hili hayati Baba wa TaifaMwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume Rais waKwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  kuendelea  kuvurungwa na wanasiasa  wachache wasiopenda amani ya nchi  hii .

Akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.com kwa njia ya  simu kutoka jijini Dar es salaam ambako amealikwa kwa  huduma za kanisa , askofu Dr  Solloa  alisema  kuwa tayari  kanisa lake  limeanza kufunga na kuomba kwa ajili ya amani nchini na kuliombea  bunge  hilo la katiba  ili mwenyezi  Mungu  kuliunganisha  bunge  hilo na kuepusha mgawanyiko  ulioanza  kujitokeza na kundi   hilo la wana Siasa wanaojiita  wana UKAWA .

" Watamzania tulipongeza uteuzi  wa Rais wetu mpendwa Dr Jakaya Mrisho  Kikwete kwa  kuteua  miongoni mwa  watanzania  wachache kati  ya  wengi kwa ajili ya kwenda kushiriki  bunge  hilo kuandaa katiba ya nchi huku  tukiamini  kuwa walioteuliwa wangetufikisha pazuri zaidi tofauti na ilivyo  sasa ambapo wajumbe  hao  wameanza kuhatarisha amani na utulivu nchini "

Kitendo  cha  wajumbe  wa bunge  hilo kutoka nje ya ukumbi na kutaka kuanza  kuzunguka mikoani ni sawa na kuwasaliti  wananchi  ambao walikuwa  wakisubiri kwa hamu wajumbe hao kuwaletea katiba mpya ila  sasa wameanza kutishia amani ya nchi kwa kutafuta  huruma ya  wananchi katika kuungwa mkono wao  na  vyama  vyao.

" Ushauri wangu kwa mheshimiwa Rais Dr Kikwete  ni kulivunja kabisa  bunge  hilo ili kunusuru amani ya nchi  hii ambavyo  dalili ya  kuvurugwa imeanza  kujitokeza kupitia UKAWA ....tulitegemea wajumbe  hao wangebaki ndani ya bunge na kutuandalia katiba  bila kuunda umoja wa  kuanzisha  vurugu nchini kwani wote  bila kujali vyama vyao na taasisi  zao  walizotoka walipaswa  kuwa kitu  kimoja katika  bunge  hilo kwa kuwasilisha hoja za kuwa na katiba  bora si vinginevyo "

Alisema  kuwa ni  vema kuendelea na katiba  iliyopo kuliko  kusubiri katiba ya  wajumbe hao ambayo mwelekeo  wake  si mzuri  bali  upo kwa ajili ya matakwa ya wachache  kisiasa .

Askofu  huyo  alisema  kuwa wananchi wa Zanzibar wanachanganywa na wana siasa  hao  ila ukweli wazanzibar   na  watanzania  wanapenda  kuona amani iliyopo  inaendelea  kuwepo na suala la maendeleo linaendelea  na sio utitiri  wa serikali hali maisha  yao kiuchumi ni duni .

Hata  hivyo  alisema kutokana na mwenendo  wa  bunge  hilo kwa  sasa  kanisa lake  limetangaza mfungo wa maombi maalum kwa ajili ya Tanzania  ili kuepuka chuki kupandikizwa na wachache kwa lengo la kuvuruga amani  yetu .
source. francis godwini.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog