Akizungumza na mtandao huu askofu boaz sollo amesema msako huo unakuja baada ya kuona watu wengi wanaonewa sana na shetani hivyo ametoa wito kwa watu wote kuungana nae katika kuvunja na kubomoa ngome zote za shetani ambaye amekuwa akiwatumikisha watu.
uzinduzi wa operation hiyo utafanyika katika ukumbi wa huduma hiyo unaoendelea kujengwa katika mtaa wa zizi la ng'ombe ambapo hadi sasa ukumbi wa awali unatarajiwa kukamilika muda wowote kuanzia sasa
askofu boaz sollo ambaye pia ni mkurugenzi wa kituo cha redio mkoani iringa ameendelea kufanyika baraka kwa wakazi wa mikoa ya nyanda za juu kusini pamoja na kati ambao wamekuwa wakimshukuru kwa jinsi ambavyo mungu amekuwa akimtumia kwa viwango vya hali ya juu.
zifuatazo ni picha za makitaba
![]() |
![]() |
. |
![]() |
0 comments:
Post a Comment