Home » »

KANISA LA WINNERS CHAPEL LA MAMILIONI LIPO KATIKA HATI HATI YA KUBOMOLEWA NA SERIKALI

[Image]
Winners Chapel la jijini Nairobi muonekano wa ndani.
Kanisa kubwa la kisasa la Winners Chapel la jijini Nairobi nchini Kenya liko kwenye hati hati ya kubomolewa na serikali ya nchi hiyo, kwa madai ya kiwanja lilipojengwa kanisa hilo ni mali ya serikali na kwamba kanisa hilo lilifanya makosa kujengwa mahali hapo.

Kanisa hilo lenye uwezo wa kubeba waumini elfu kumi na wanane (18,000) kwa wakati mmoja ambalo ujenzi wake umechukua miaka tisa hadi kukamilika kwake likiwa limejengwa eneo la south B estate huku likitajwa kuwa ni moja kati ya makanisa bora kujengwa Afrika mashariki na kati liko chini ya kanisa mama la Winners Chapel lenye makao makuu yake nchini Nigeria chini ya kiongozi na mwanzilishi wake mchungaji David Oyedepo anayetajwa kuwa mmoja kati ya watumishi wa Mungu matajiri duniani.

[Image]
Winners Chapel la jijini Nairobi nchini Kenya, katika muonekano wa nje.©skyscrapercity
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari vya nchini Kenya vinasema kwamba katibu mkuu wa kilimo, ufugaji na uvuvi wa kenya bwana Felix Kosgey amesema serikali itatoa siku 21 kwa wamiliki wa nyumba hizo katika kiwanja cha diamond park ambacho kimejengwa nyumba mbalimbali za kifahari pamoja na south B ambako kumejengwa kanisa hilo kuondoka ili zibomolewe tayari kwa matumizi mengine ya serikali.

Kiwanja hicho chenye jumla ya ekari 210 kimezua mzozo na kufikia wakazi wake kufika ofisini kwa meneja mradi wa nyumba hizo Ahmed Rashid ili kupata ufafanuzi juu ya kauli iliyotolewa na bwana Kosgey. Ambapo kwa mujibu wake meneja huyo amesema toka kutolewa kwa kauli hiyo wamekuwa katika wakati mgumu kutoka kwa watu hao na wengine wakipiga simu kutoka nje ya nchi wakiulizia uhalali wa eneo hilo ambalo amesema lina nyumba zipatazo 600 ambazo zipo katika eneo hilo kwa miaka 10 sasa huku kila nyumba ikiwa inathamani ya shilingi milioni 16 za Kenya huku wengine wakiwa wamiliki na wengine wapangaji katika nyumba hizo.

[Image]
Mchungaji Oyedepo katikati na mkewe sambamba na makamu wa Rais wa Kenya bwana William Ruto wakikata keki wakati wa uzinduzi wa kanisa hilo ambalo lipo katika hatihati ya kubomolewa.©gadiola25
Kwa upande wa mmoja wa wachungaji wa kanisa la Winners ambaye hakupenda jina lake litajwe kwakuwa si msemaji wa kanisa ameiambia Nairobi news kwamba kabla hawajaanza ujenzi wa kanisa hilo waliwakilisha nyaraka zote muhimu kwa vyombo husika.




[Image]
Nyumba ambazo zipo katika hatihati ya kubomolewa katika eneo la Diamond Park jijini Nairobi ©nairobinews
[Image]
Moja ya ndege ya kifahari ya kiongozi wa kanisa la Winners duniani David Oyedepo.©dailymail
[Image]
Mchungaji David Oyedepo akiwa ndani ya ndege yake, akifurahia jambo.©dailymail
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Search This Blog