Home » »

NYOTA WA MUZIKI WA INJILI UGANDA AFA AKIOGELEA TANZANIA

Marehemu Mark Elvis enzi za uhai wake.
Wapenzi wa muziki wa injili jijini Kampala nchini Uganda hasa wa kanisa la Watoto, wameshikwa na mshtuko baada ya kusikia kifo cha aliyekuwa nyota wa muziki wa gospel nchini humo kijana Mark Elvis Mutalya au kwakifupi mwite Mac Elvis (26) a.k.a church boy kilichotokea jijini Dar es salaam juzi ijumaa baada mwimbaji huyo aliyekuwa katika ziara ya kihuduma na waimbaji wenzie wa injili katika shule mbalimbali jijini Dar es salaam kuzama kwenye bwawa la kuogelea(swimming pool) maeneo ya Mbezi.

Marehemu ni mmoja kati ya watoto yatima waliolelewa na kanisa maarufu la Watoto nchini Uganda baada ya wazazi wake kufariki akiwa na miaka sita tu, ambapo alichukuliwa na kanisa la Watoto ambao walimpeleka shule na kuhitimu elimu ya juu ya sekondari na ndoto yake toka wakati huo ilikuwa kuingia kwenye muziki, ndoto ambayo ilitimia kama alivyotaka na kujikuta akipata umaarufu baada ya nyimbo zake kushika nafasi za juu katika radio mbalimbali nchini Uganda.

Kaka wa marehemu aitwaye Ivan ambaye alikuwa ni mmoja kati ya watoto wa kwanza wakati huduma ya Watoto inaanza mwaka 1994 naye alifariki dunia miaka michache iliyopita. Kutoka na hayo yote Elvis aliamua kumwachia Mungu maisha yake na kila kitu alichonacho hasa katika kumwimbia yeye kutokana na  tumaini na upendo alioupata kutoka kwa Yesu, kuliko kufikiria machungu anayopitia.

Katika moja ya mashairi ya nyimbo zake Elvis aliimba"If I were to change anything about my life, I wouldn't change a thing. It's what I experienced in the past that moulded me into who I am today," he always remarked in interviews. "It's been God's grace, love and care that has carried me through."
Mpaka umauti unamkuta kijana huyo ana album tatu ya kwanza inayoitwa "Your love"aliitoa mwaka 2009, Church boy(2011) na hivi karibuni aliachia single zake katika album mpya ijayo moja ya nyimbo hizo ni Topowa game unaopendwa kwenye vituo vya radio na televisheni nchini kwake.

Kati ya mafanikio aliyopata katika muziki wa injili tangu aingie rasmi mwaka 2006 ni pamoja na tuzo za Uganda Olive Awards, pamoja na kutajwa kwenye tuzo za Grooves za Kenya kama mwimbaji bora kutoka Uganda. Lakini pia ameimba kama mwimbaji mtangulizi katika matamasha ya waimbaji wakubwa wa gospel duniani waliofika Kampala Uganda kama Kirk Franklin, Papa San,Sean Slaughter na Cece Winans.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Search This Blog