LIVING WATER YAITEKA SHINYANGA
Huduma ya Living Water Centre Ministry chini ya mtumishi wa Mungu
Apostle Onesmo Ndegi yenye makao yake makuu Kawe Jijini Dar es Salaam
wikiendi iliyokwisha ilikuwa ikihitimisha mkutano wa Injili katika
Kanisa lake Mkoani Shinyanga.
Semina hiyo ilidumu kwa siku 5 na Apostle Ndegi aliyekaribishwa na
mwenyeji wake Mch. Nazareth Manase wa Living Water Centre Shinyanga,
Mkutano huo ulio uliohudhuriwa na watu wengi kutoka katika kila kona za
mji wa shinyanga kuja kusikiliza Neno la Mungu.
Katika Mkutano huo waimbaji wa Nyimbo za...
Posted by Unknown
Posted on 5:19 PM
with No comments

MSIBA WA ASKOFU KULOLA KUWA EAGT TEMEKE, MWILI KUSAFIRISHWA MWANZA, FLORA MBASHA AZIMIA
Taarifa za mwendelezo kuhusu msiba wa Askofu Dr. Moses Kulola zinasema
kuwa msiba utakuwa kanisa la EAGT Temeke kwa Mchungaji Ngowi, mahali
ambapo kila mwaka amekuwa akifanya mkutano wa injili, na kwamba kwa wale
ambao watapenda kuhudhuria wafike mahali hapo.
Mwili wa Askofu Kulola tayari umehamishwa kutoka hospitali ya AMI kwenda
Hospitali ya Kumbukumbu ya Hurbet Kairuki iliyopo Mbezi jijini Dar.
Mwili utasafirishwa kuelekea Mwanza, na mipango ya shughuli hiyo bado
inafanyika.
Kwa mujibu...
AMBWENE MWASONGWE NA TUMSIFU RUFUTU, FREDY NDUMBALO KUITIKISA IRINGA WIKI HII
Posted by Unknown
Posted on 7:47 AM
with No comments

albamu mpya ya ambwene mwasongwe ambaye pia anatarajia kutikisa mji wa iringa wiki hii
Tumsifu rufutu pichani akiimba wimbo wake wa mwambie farao katika moja kati ya mikutano yake.
Wiki hili kuanzia alhamisi wakazi wa iringa watapata baraka za mwaka kutoka kwa waimbaji wa injili ambwene mwasongwe pamoja na tumsifu katika kongamano la maombi na maombezi linalotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa mwembetogwa manispaa ya iringa
mkutano huo unaosubiriwa kwa hamu mhubiri ni mtume na nabii ezekiel fungo kutoka jiji la mwanza ndiye atalkaye hubiri gospel za iringa itaendelea...
Posted by Unknown
Posted on 7:08 PM
with No comments

MASANJA AMPONGEZA MATUMAINI KUOKOKA AMTAKA KUFUMUA BREKI ZOTE ILI ASONGE MBELE
Masanja kushoto akiwa na pacha wake Silas Mbise.
Wiki moja tangu mchekeshaji maarufu nchini aitwaye Matumaini kutoa wimbo
wake wa kwanza wa injili wa kumshukuru Mungu kwa kumponya na ugonjwa
mbaya ambao ulimpata akiwa nchini Msumbiji, mchekeshaji mwenzake
Emmanuel Mgaya a.k.a Masanja Mkandamizaji amempongeza mwigizaji mwenzake
huyo kusonga mbele na kutokatishwa tamaa na watu wengine juu ya uamuzi
wake wa kumpa Kristo maisha yake.
Masanja amesema anajua Matumaini ametendewa jambo kubwa na Mungu la
uponyaji...
Posted by Unknown
Posted on 1:23 PM
with No comments

MAKALA : SIZE 8 ALIKOSA AMANI MOYONI KUIMBA NYIMBO ZA KIDUNIA
Tarehe 12 April mwaka huu ilikuwa siku ya kipekee sana kwa wapenzi wa
muziki wa gospel na wale ambao wameokoka baada ya mwimbaji maarufu
aliyekuwa akitengeneza pesa nyingi na kupendwa na mashabiki wa muziki wa
nje ya kanisa kuamua kumrudia Mungu wake na kutangaza kuachana na
muziki huo aliokuwa akiufanya awali na kurudi kanisani.
Huyu si mwingine bali mwanadada Linet Munyeli ama mwite size 8 jina lake
maarufu huyu ni mwimbaji wa gospel kutoka pale nchini Kenya, mwimbaji
huyu aliyetamba na nyimbo mbalimbali nchini humo...
Posted by Unknown
Posted on 1:07 PM
with No comments

UTAJIRI WA DHULUMA NA KAFARA HAUNA BARAKA WALA AMANI
Askofu Paul Akyoo. picha kwa hisani ya elct.org
Askofu Paul Akyoo wa Dayosisi ya Meru kanisa la Kilutheri nchini
amekemea vikali utajiri wa dhuluma na kafara kwakuwa hauna baraka.
Askofu Akyoo ameyasema hayo hapo jana wakati wa ibada ya mazishi ya
mfanyabiashara maarufu wa madini ya Tanzanite jijini Arusha marehemu
Erasto Msuya aliyefariki kwakupigwa risasi Agosti 7 mwaka huu.
Askofu Akyoo katika mahubiri yake alisema utajiri wa dhuluma na kafara
hauna baraka wala amani kwa wahusika kutokana na dhamira zao kuwasuta
kila wanapokumbuka...