Home » » MARTHA MWAIPAJA NA CHRISTINA SHUSHO NDANI YA LONDON, WAPIGIE KURA YAKO

MARTHA MWAIPAJA NA CHRISTINA SHUSHO NDANI YA LONDON, WAPIGIE KURA YAKO

MARTHA MWAIPAJA NA CHRISTINA SHUSHO NDANI YA LONDON, WAPIGIE KURA YAKO



Martha Mwaipaja nyota yake imeonekana kung'ara na kutambulika kimataifa baada ya kupendekezwa kwa mara ya kwanza kuwania tuzo za injili za Afrika ziitwazo Africa Gospel Music Awards(AGMA) ambazo zinatarajiwa kutolewa mapema mwezi wa saba mwaka huu jijini London.

Mwimbaji huyo anayetamba na album yake ya pili aliyoitoa mapema mwaka jana amewekwa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania tuzo ya mwimbaji wa mwaka Afrika mashariki akiwa sambamba na nyota mwingine wa muziki wa injili nchini Christina Shusho ambaye amependekezwa kuwania tuzo hizo kwa mara ya tatu mfululizo. Waimbaji hawa pekee kutoka Tanzania watakuwa wanawania tuzo hiyo na waimbaji wengine kutoka Kenya na Uganda.
Christina Shusho.


Kama ilivyokuwa kwa mwaka jana ambapo blog za Kikristo nchini tuliendesha kampeni ya kumwezesha Shusho kutwaa tuzo hiyo lakini kura hazikutosha, kwa mwaka huu tunao waimbaji wawili kutoka
nchini, ukiwa kama Mtanzania na mwana Afrika Mashariki tunaomba chukua muda wako wa dakika zisizopungua tano kuwapigia kura waimbaji wetu.

Wanaowania tuzo ya mwimbaji wa mwaka Afrika mashariki ndio hawa

Eunice Njeri (Kenya)
Christina Shusho(Tanzania)
Jimmy Gait (Kenya)
Kambua (Kenya)
Jackie Senyonjo(Uganda)
Kris Eh Baba (Kenya)
Coopy Bly-Uganda
Martha Mwaipaja-Tanzania
DK Kwenye Beat(Kenya)
Eko Dydda(Kenya)

Hata hivyo katika tuzo hizo kama ilivyokawaida waimbaji kutoka nchini Kenya wameonekana kung'ara katika kuwania tuzo tofauti huku, kinyang'anyiro kikali kinategemewa kuwa kusini mwa bara la Afrika ambako waimbaji nyota wa Afrika ya kusini wanawania tuzo hizo pia. Ambapo katika kinyang'anyiro hicho mwimbaji nyota kutoka kundi la Joyous Celebration Charisma Hanekam anatarajiwa kuwa mmoja wa waimbaji siku ya kutolewa kwa tuzo hizo zitakazofanyika tarehe 6/7/2013 katika ukumbi wa The Great Hall, Queen Mary jijini London nchini Uingereza.

Kungalia vipengele mbalimbali vya tuzo na waimbaji waliopendekezwa ikiwa pamoja na upigaji kura BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Search This Blog