Home » »

KWA TAARIFA YAKO : MASWALI MENGI KUHUSU NDOA YALIMFANYA MARION SHAKO KUDANGANYA

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu cha ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina ukweli utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu


KWA TAARIFA YAKO hii leo tupo kwa mwanadada aliyetokea kuteka masikio ya wakazi wa Afrika Mashariki kupitia wimbo wake "AHADI ZAKE" uliomtambulisha vyema na kumpatia tuzo huko nchini kwao Kenya, huyu si mwingine bali ni Marion Wyali Shako.

KWA TAARIFA YAKO kama ukuwahi kufahamu hili au kusoma makala tuliyowahi kuandika kuhusu mwimbaji huyu na wimbo wake wa huo ambao wengi waliousikia mara ya kwanza walidhani mwimbaji ni Beatrice Muhone ni kwamba, kupitia Wapo Radio Fm akihojiwa katika kipindi cha ''Safari ya jioni'' alisema wimbo wa AHADI ZAKE ambao upo ndani ya album yake ya ''MSAADA WANGU'' alipewa neno la kinabii na nabii Teresia Wairimu kwamba Mungu atampa wimbo utakaobadilisha maisha yake na watu wengine,wakati anapewa unabii huo alikuwa katika hali ya uhitaji sana na album yake hiyo mpaka anaifanikisha kuirekodi ni Mungu mwenyewe alimsimamia kwani alimaliza salio lake lote alilokuwa nalo na pia alipitia mapito magumu sana.


KWA TAARIFA YAKO Marion Shako ambaye licha ya kuwa ni mwajiriwa pia anajihusisha na biashara huko kwao Mombasa Kenya  kutokana na kupata maswali mengi ya watu kila anakokwenda kuhudumu kuhusu lini ataolewa ilibidi adanganye kwenye moja ya shoo ya mchekeshaji maarufu wa Kenya aitwae Churchill ambako aliulizwa swali kuhusu harusi yake lini bila kusita Marion alijibu itakuwa hivi karibuni kitendo ambacho alijutia baadae kwakuwa alidhani amepunguza maswali kumbe ndio yalikuwa yameongezeka na watu kutaka kujua undani zaidi wa harusi yake itafanyika lini na ninani muhusika mkuu, kitendo cha kuulizwa sana maswali ikabidi aweke jibu hadharani kwamba hawezi kuzungumzia masuala yake ya uhusiano hadharani na kwamba hategemei kufunga harusi kwa mwaka huo(ilikuwa 2011, GK haijui kama amefunga kwasasa pia) na kusema kwamba aliamua kusema anafunga harusi karibuni ili kuwaridhisha mashabiki na watu waliokuwa wakimuuliza maswali hayo kwakuwa walitaka jibu kama hilo. kama alivyofafanua kwenye mahojiano na gazeti la The Star

Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Search This Blog