Home » » Mzee Majuto : Ntaendelea Kuigiza Hadi Siku Yangu ya Kifo Changu

Mzee Majuto : Ntaendelea Kuigiza Hadi Siku Yangu ya Kifo Changu

Mkongwe wa Filamu za Kibongo nchini, aliyejipatia umaarufu kwa kuigiza vichekesho, Amri Athumani ‘Mzee Majuto’, aliyeanza kuagiza mwaka 1958 akiwa na miaka 10, ambaye mwaka jana aliwahi kutangaza kuacha uigizaji na kumrudia Mungu, amesema ataendelea kuigiza hadi anakufa kwa sababu uigizaji upo kwenye damu na hii inadhihirishwa wazi kwani ni miaka 58 sasa ya uigizaji wake na fani hii ameianza akiwa darasa la pili.

Majuto alizungumza hayo Dar es salaam Jana.Alisema hawezi kukubali kuona fani inachezewa na watoto, hivyo ataendelea kuigiza hadi siku atakayokufa kwa sababu uwezo wake ni wa hali ya juu kwenye kuandika na kuigiza.

”Kuigiza kwangu ni kama maradhi vile, hivyo sidhani kama naweza kuacha, siwezi kukaa pembeni  sanaa ikawa inachezewa na watoto sitaki kabisa,  nitaendelea kuigiza hadi nakufa,” alisema Majuto.

Mzee Majuto aliongeza ataendelea kuigiza  ili kuhakikisha anapata chipukizi ambaye anaweza kufanya kile alichokuwa anakifanya yeye hapo baadae.

Alisema bado hajapata mtu wa kurithi mambo yake katika tasnia hiyo, hivyo hawezi akakurupuka kuachana na kazi hiyo bila ya faida ambayo kwa upande wake ni kupata mrithi.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog