Home » » DC KILOLO AMFUKUZA MKUU WA KITUO CHA POLISI MTITU .

DC KILOLO AMFUKUZA MKUU WA KITUO CHA POLISI MTITU .

                           NA DENIS NYALI IRINGA
Kufuatia kuripotiwa kwa wingi wa matukio ya ubakaji mkoani iringa na tanzania kwa ujumla mkuu wa wilaya ya kilolo  Mh Asia abdallah ameagiza kuhamishwa mara moja mkuu wa kituo cha mtitu kilichopo wilaya ya kilolo kutokana na uzembe wa kutofikisha taarifa za tukio la ubakaji kwa mkuu wa kituo cha polisi wilaya .

Tukio hilo limetokea baada ya mtoto mwenye umri wa miaka mitano na nusu kubakwa na watu watatu katika kijiji cha mawambala na kuharibiwa vibaya sehemu ya mwili wake.
Akizungumzia Tukio hilo la kikatili lilotokea katika kijiji cha mawambala kata ya ukumbi wilaya ya kilolo mkoani iringa afisa mtendaji wa kijiji hicho NOLASCO KIHWELO  amesema taarifa juu ya tukio hilo zimelipotiwa na mama wa mtoto huyo.
Mtendaji wa kijiji ameongeza kuwa baada ya kupokea taarifa hizo yeye pamoja na wazazi hao wakishirikiana kumkamata mtuhumiwa mmoja huku wengine wawili wakikimbilia kusikojulikana.
Akizungumza kwa uchungu mama wa mtoto huyo amesema alikuwa akipika jikoni ndipo baba mdogo wa mtoto huyo alipo mwona mtoto huyo akishindwa kutembea na ndipo mama yake alipofika na kumkuta tayari ameshafanyiwa ukatili huo.

NAYE  mtoto aliyefanyiwa ukatili huyo ambaye hajui lugha ya Kiswahili akizungumza kwa lugha ya kihehe amesema watuhumiwa waliotekeleza kitendo hicho walimtisha kuwa asimwambie mtu na endapo akisema watamkata kwa panga.

           
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Search This Blog