Home » » HABARI ZAIDI ZA PADRI ALIYEPIGWA RISASI ZANZIBAR USIKU WA JANA

HABARI ZAIDI ZA PADRI ALIYEPIGWA RISASI ZANZIBAR USIKU WA JANA


HABARI ZAIDI ZA PADRI ALIYEPIGWA RISASI ZANZIBAR USIKU WA JANA

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Aziz Juma Mohammed amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo alisema Father amepigwa risasi na ameumizwa sehemu ya kichwa na amekuwa akitoka damu nyingi kichwani na tayari anapatiwa matibabu katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja.
Alisema jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini wahusika walifanya uhalifu huo kwa madhumuni gani kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

“Sisi tunahesabu kuwa kitendo hiki ni kitendo cha kihalifu na tunawatafuta wahalifu waliofanya kitendo hiki kwa hivyo bado ni mapema kusema kwamba kitendo hiki kimefanywa na nani kwa kuwa bado uchunguzi wetu unaendelea na hadi sasa hakuna mtu tuliyemshika kuhusikana na tukio hili” alisema Kamanda.



Kamanda Aziz akisimulia tukio hilo alisema walipata taarifa majira ya saa 2 na kwenda katika eneo la tukio ambapo Father alikuwa akitokea kanisani na kutaka kuelekea nyumbani kwake wakati akiwa ndani ya gari ndipo aliposhambuliwa na watu wasiojulikana na kuanguka.

“Tumekuta mabaki ya risasi ndani ya gari yake na katika vioo vyake vya gari vimevunjika na tumekuta damu chini pale” alisema Kamanda.

Aidha Kamanda Azizi alisema Father Ambros yeye ni mhasibu pale kanisani na hivyo mara nyingi watu wananaamini kwamba katika siku za krismass mara nyingi sadaka hukusanywa fedha nyingi na hivyo wanamini kwamba alikuwa fedha mikononi na ndipo inawezekana waliamua kumpiga risasi wakitaka kuchukua fedha hizo.

Hata hivyo alisema uchunguzi wa awali ndio utakaoeleza ni suala gani lililopelekea kupigwa risasi lakini wanaendelea na uchunguzi huo ambapo uchunguzi ndio utakaojulikana sababu kamili ya tukio hilo.

Akizungumzia tukio hilo, Askofu Michael Hafidh wa Kanisa la Anglikan la Mkunazini amesema wamesikitishwa na wamepokea kwa mshituko mkubwa tukio hilo hasa kwa kuzingatia matukio kama hayo hayajawahi kutokea ya kuwahujumu viongozi wa dini.


Alisema tukio hilo ni miongoni mwa matukio ya kushtusha na yanaashiria hali mbaya ya kiusalama na kuwaomba viongozi wa serikali kuchukua hatua za tahadhari kubwa kwani matukio kama hayo yameanza kutokea kwa viongozi wa dini ambapo mwanzo ilianzia kwa Sheikh Soraga na baadae kutokea kwa Father Ambros.

“ Hii ni hali ya hatari katika nchi yetu na haipendezi lakini serikali lazima ijue sisi hatuwezi kujua wala hatuwezi kujilinda lakini serikali inapaswa kutulinda sisi ndio wananchi wake” alisema Askofu Hafidh.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Search This Blog