IRINGA
Watu wawili wanashikiliwa na
jeshi la polisi kwa kosa la kumlawiti
mtoto wa miaka 7 mwanafunzi wa shule ya msingi umoja, mtwivila manispaa ya
Iringa.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Iringa
ACP RAMADHANA ATHUMAN MUNGI amesema mtoto huyo amelawitiwa na watu wawili baada
ya kumkamata na kumuingiza katika chumba na kwamba Jeshi la polisi limefanikiwa kumkamata
mtuhumiwa mmoja anaefahamika kwa jina la JOHN LUCAS mwenye umri wa miaka 25.
Wakati huohuo kamanda Mungi amethibitisha kukamatwa kwa mtu mmoja
ambaye ni mkazi wa kijiji cha mapogolo anaefahamika kwa jina la ADAM
MBILINYI kwa kosa la kuvunja nyumba ya
mwanamke na kumbaka.
Kamanda Mungi amewataka watu wenye tabia za ulawiti na ubakaji kuacha
tabia hizo kwa kuwa zinadhalilisha utu wa mtu na kwamba Jeshi la polisi
halitawafumbia macho wale wenye tabia
hizo.


0 comments:
Post a Comment