Kama hujawahi kukutana na kichwa cha habari kinamchomtaja Jumanne Kishimba, basi taarifa ikufikie kwamba kwenye list ya Wabunge wataowakilisha Dodoma kwenye Bunge la 11 na yeye yumo.
Jumanne Kishimba ni Mbunge mteule wa Jimbo la Kahama, lakini aliwahi kuandikwa pia kutokana na elimu yake ya darasa la saba !!
Amepatikana kwenye exclusive interview na reporter wa millardayo.com, akaanza na stori kuhusu safari yake Kisiasa ilikoanzia >>> ‘Nawashukuru
sana wapiga Kura wa Kahama kwa kunichagua, nilijaribu mwaka 2000 wakati
Jimbo la Msalala halijagawanywa lakini tulifutwa Wagombea wote wa CCM
kulikuwa na rafu kidogo tulicheza. Toka mwaka 2000 sikuwahi kugombea
mpaka mwaka huu 2015‘ >>> Jumanne Kishimba, Mbunge mteule Jimbo la Kahama.
Jumanne Kishimba aliwahi kuendelea kuiwaza Siasa baada ya kushindwa kwa mara ya kwanza? >>> ‘Imekuwa
kwenye ndoto zangu kwa kuwa biashara na siasa ni kama mtu na ndugu
yake, kulikuwa na mvutano mkubwa kwa kuwa elimu yangu ni darasa la saba
lakini nina uzoefu wa kutembea sehemu nyingi na nimefanya kazi nyingi,
ni vizuri kukawa na mchanganyiko wa wenzetu wenye elimu na sisi wenye
uzoefu tukatatua changamoto pamoja Bungeni‘. >>>
Anazijua changamoto za wananchi wake? >>> ‘Wananchi
wangu wanahitaji dawa, dispensary, maji, umeme.. ni vitu ambavyo elimu
ya darasa la saba kwa Mbunge sio tatizo, Bungeni huendi kufanya
operation kwamba unaweza kuua watu. Bungeni ninapeleka mawazo ya
walionituma na kuongeza ya kwangu kwa kuwa una uzoefu‘. >>> Jumanne Kishimba.


Daaaaaaaah nimecheka sana kaka
ReplyDeleteAtakuwa msomi tu kwa Magufuli