Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Dodoma SACP David Misime---
Polisi
Mkoa wa Dodoma inawashikilia wanafunzi 84 wa chuo Kikuu UDOM kwa tuhuma
za kuhamasisha uvunjifu wa amani Chuoni na kufanya maandamano haramu
kutoka Chuoni kuelekea katika Ofisi mbalimbali za viongozi wa Serikali
zilizopo Dodoma Mjini tarehe 14.01.2015 majira ya 05:30 (kumi na moja
alfajiri).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi SACP David Misime ameeleza kuwa chanzo cha
wananfunzi hao wa programu maalum ya diploma ya Ualimu kufanya uhalifu
huo ni kikao walichofanya wananfunzi hao tarehe 13.01.201 wakidai
kuongezewa posho ya chakula na kwamba hata kiasi ambacho wanapewa
wamechelewa kupewa.
Hata hivyo uongozi wa Chuo uliwaeleza kuwa wenye
mamlaka ya kuzungumzia swala la kuongezewa posho ni Bodi ya Mikopo na
siyo chuo. Hivyo walitakiwa kufuata taratibu za kuwasilisha madai yao.
Pia walielezwa kuwa hundi kwa ajili ya fedha za posho zao zimeshasainiwa
na kuwasilishwa Benki ili waweze kuanza kupewa posho zao.
Hata hivyo
wanafunzi hao hawakuridhika na usiku wakaanza kuhamasishana kufanya
maandamano jambo ambalo ni kosa kisheria. Wanafunzi hao wamehojiwa
kulingana na ushahidi ambao umekusanywa na wamefikishwa mahakamani kwa
kosa la Kufanya Maandamano yasiyo na kibali. Viongozi waliohamasisha
uvunjifu huo wa sheria baadi wamekamatwa na baadhi wanaendelea kutafutwa
ili nao waweze kuchukuliwa hatua stahiki.
Ushahidi uliokusanywa
unaonyesha jinsi viongozi hao wameshiriki kuhamasisha kupitia vikao
rasmi na visivyo rasmi, katika vikundi, kupita katika mabweni na kutuma
sms.Kamanda wa Polisi ametoa wito kwa Wanafunzi hao kutumia taratibu
zilizowekwa na Serikali na Chuo kuwasilisha malalamiko yao ngazi kwa
ngazi na siyo kufanya vitendo vya kuvunja sheria ambavyo
vitawasababishia kukamatwa.
Endapo watafanya hivyo wasije kulaumu mtu
kwani hatua zitachukuliwa kulingana na Sheria inavyoelekeza ikiwa ni
pamoja na kufikishwa mahakamani. Imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Dodoma. Baadhi
ya Wanafunzi 84 wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakiwa chini ya ulinzi
kwa tuhuma za kuhamasisha uvunjifu wa amani Chuoni hapo na kufanya
maandamano haramu kutoka Chuoni kuelekea katika Ofisi mbalimbali za
viongozi wa Serikali zilizopo mjini Dodoma .Baadhi
ya Wanafunzi 84 wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakiwa kwenye gari ya
polisi baada ya kutiwa mbaroni kwa tuhuma za kuhamasisha uvunjifu wa
amani Chuoni hapo na kufanya maandamano haramu kutoka Chuoni kuelekea
katika Ofisi mbalimbali za viongozi wa Serikali zilizopo mjini Dodoma
0 comments:
Post a Comment