BREAKING NEWS..!! KITUO CHA POLISI IKWIRIRI MKOANI PWANI CHAVAMIWA NA MAJAMBAZI, ASKARI WAWILI WAUWAWA
Mfano wa bunduki aina ya SMG zilizoibiwa.
MAJAMBAZI
yaliyojihamu kwa silaha yamevamia Kituo cha Polisi cha Ikwiriri, Rufiji
mkoani Pwani na kuua askari wawili na kupora silaha zilizokuwepo
kituoni hapo.
Tukio
hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, huku askari wanaodaiwa kupotenza
maisha ni Cop. Edgar aliyekatwa mapanga na WP Judith aliyepigwa risasi
ubavuni upande wa kulia na kutokea upande wa kushoto.
Hivi
sasa hali ni tete katika eneo hilo na watu wamekusanyika huku polisi
wakiongeza nguvu kusaka wauaji katika tukio la uvamizi, kituo cha polisi
Ikwiriri, Rufiji, Pwani.
Silaha zilizoporwa ni SMG 2, SAR 2, SHORTGUN 1, silaha 2 za mabomu ya machozi na risasi 60 za SMG.
0 comments:
Post a Comment