POLISI WAUA MAJAMBAZI WAWILI JIJINI DAR ES SALAAM BAADA YA KURUSHIANA RISASI
Jeshi la Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kukamata silaha moja aina ya SMG
yenye namba BA172288 na risasi 13 wakati wa mapambano makali ya ana kwa
ana kati ya majambazi na Jeshi la Polisi.
Taarifa
iliyotolewa na jeshi hilo Kanda Maalum ya Dar es salaam, imesema kuwa
katika tukio hilo majambazi wawili waliuawa kwa risasi wakati wakijaribu
kuwadhuru askari.
Tukio hilo lilitokea eneo
la Kariakoo mtaa wa Mkunguni na Livingstone saa 3.00hrs usiku wa jana.
Wakati wa tukio hilo umeme ulikuwa hakuna na mlalamikaji alikuwa
anatumia taa za kawaida.
Mara baada ya kuanza
tukio hilo la uporaji wasamaria wema walijulisha Jeshi la Polisi ndipo
kikosi maalum cha kupambana na majambazi (ant robbery squared)
kilipofika kwa haraka katika eneo la tukio tayari kwa mapambano.
Taarifa hiyo inasema kuwa
Majambazi hao walistuka na kuanza kuwarushia risasi askari waliokuwa
katika gari la Polisi na ndipo sasa kukawa na mapambano ya moja kwa moja
kati ya pande hizo mbili kwa kutumia silaha na kurushiana risasi.
Hatimaye majambazi wawili
waliuawa, mmoja anayejulikana kwa jina la ALLAN S/O OCHENG @ ONYANGO,
Miaka 24, raia wa Kenya alipatikana na Pass ya kusafiria yenye nambari
A1688495 iliyotolewa katika mji wa KISUMU nchini Kenya.
Jambazi mwingine
aliyeuawa ametambuliwa kwa jina la YUSSUPH S/O HAMIS @ TWALIB, Miaka 46,
Mshiraz, Mkazi wa Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Majambazi wengine
waliotoroka baada ya tukio hilo wanaendelea kutafutwa na tunaomba raia
wema waendelee kushirikiana na Jeshi la Polisi ili wapatikane.
Pamoja na kuuawa kwa
majambazi hawa na kukamatwa kwa silaha, pia zimekamatwa pikipiki mbili
moja ni SUNLG yenye namba za usajili T249 CMC, rangi nyekundu. Nyingine
ni aina ya BOXER yenye namba za usajili MC350 AM rangi nyeusi ambazo
zote zilitumiwa na majambazi hao katika tukio.
Aidha, Jambazi ALLAN S/O OCHENG @ ONYANGO aliyeuawa amekutwa na simu ya mkononi aina ya TECNO.
Majambazi Wengine 9 Sugu Wakamatwa jijini Dar
Katika msako mkali
unaoendelea jijini Dar es Salaam dhidi ya ujambazi wa kutumia silaha
Jeshi la Polisi limekamata majambazi tisa wanaojihusisha na matukio ya
uhalifu ya unyang’anyi wa kutumia silaha na makosa ya kuvunja nyumba
usiku na kuiba.
Oparesheni kali bado
inaendelea jijini Dar es Salaam ili kuhakikisha kwamba majambazi wote
wanaotumia silaha pamoja na makosa mengine ambayo ni kero katika jamii
yanashughulikiwa kikamilifu.
Pamoja na mafanikio hayo
tunawashukuru raia wema kutokana na juhudi zao za kutoa taarifa mapema
zenye kuwa na mafanikio ya kulifanya jiji la Dar es Salaam liendelee
kuwashwari.
0 comments:
Post a Comment