UNYAMA MKUBWA! AMUUA MKEWE, AJICHOMA KISU HUKO TABORA!
Marehemu Zuhura Juma (31) baada ya kuuliwa na mumewe.Na Leah Marco, TABORA/Uwazi
DUNIA
inazidi kwenda kubaya! Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Maulid Mussa
(35), mkazi wa Kijiji cha Igoko wilayani Uyuwi, Tabora anashikiliwa na
jeshi la polisi kwa madai ya kumuua mkewe, Zuhura Juma (31) kwa kumchoma
visu sehemu mbalimbali za mwili.
Tukio
hilo la kusikitisha lilitokea saa tisa usiku wa kuamkia Jumatatu ya
Januari 12, mwaka huu katika Kijiji cha Usagala Kata ya Magengati Tarafa
ya Puge wilayani Nzega, Tabora nyumbani kwa wazazi wa mwanamke huyo.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu, Maulid alifikia uamuzi huo mgumu baada ya mkewe
kumuuliza habari alizozisikia kuwa aliuza shamba la tumbaku la familia
bila yeye kujua hali ambayo haikumpendeza mwanaume huyo.
0 comments:
Post a Comment