MSHAURI wa masuala ya ulinzi katika Benki Kuu (BoT), Shaban Ndosi
(39) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
akikabiliwa na mashitaka ya kujaribu kumuua ofisa wa Polisi.
Ndosi alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Waliarwande Lema.
Wakili wa Serikali, Janeth Kitali alidai kuwa Oktoba 21, 2014 katika
eneo daraja la Selander karibu na taa za kuongoza magari, alijaribu
kumuua askari Polisi, Koplo Salehe.
Hakimu Lema alisema mshitakiwa hakutakiwa kujibu mashitaka kwa kuwa
mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na upelelezi
umeshakamilika hivyo kesi itahamishiwa Mahakam Kuu.
Mshitakiwa aliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa
na wadhamini wawili wa kuaminika waliosaini hati ya dhamana ya Sh
milioni mbili, pia alitakiwa kuwasilisha mahakamani hati yake ya
kusafiria.
Kesi hiyo itatajwa tena Februari 23 mwaka huu
0 comments:
Post a Comment