Matuko ya kupiga na kunyanyaswa wanawake bado yameendelea kuchukua nafasi katika nchi malimbali za Afrika.
Tumekuwa tukiona ripoti mbalimbali za matukio mabaya ya unyanyasaji, kutoka Kenya mwanaume mmoja amefunguliwa mashtaka baada ya jaribio la kutaka kumuua mke wake kwa madai alishindwa kumpatia chakula cha moto.
Mwanaume huyo Peter Muthii alimmwagia mkewe petrol akiwa amelala, akawasha moto na kumfungia ndani ambapo muda mfupi baadaye majirani walikuja kumwokoa na kumkimbiza hospitali.
Kisa cha tukio hilo kimetajwa kuwa ni baada ya mwanaume huyo kurudi nyumbani usiku na kumtaka mkewe kumpashia chakula lakini mkewe alimwambia apashe mwenyewe kitendo kilichomkwaza, akaamua kumlipua kwa kutumia petrol iliyokua chini ya kitanda chao.
0 comments:
Post a Comment