KIJANA AUAWA KWA KUCHOMWA MOTO MJINI SHINYANGA BAADA YA KUIBA NDALA.
Mwanamme
mmoja anayekadiriwa kuwa na miaka kati ya 30 hadi 32 aliyekuwa
anajulikana kwa jina la WA TABORA ameuawa kwa kupigwa kasha kuchomwa
moto na wananchi waliojichukulia sheria mkononi karibu na makaburi ya
Majengo mjini Shinyanga.Tukio hilo limetokea mchanawa leo na inaelezwa
kuwa chanzo ni mwanamme huyo kutuhumiwa kuiba sandals(ndala)
Mwili wa marehemu ukiwa katika shamba la bibi Jeni Kiweru karibu na makaburi ya majengo mjini Shinyanga
Inaelezwa kuwa aliyeuawa alikuwa na tabia za wizi na mara kwa mara alikuwa anapigwa kwa tabia zake na leo zimetimia za mwizi 40.
Wakazi wa Shinyanga wakiangalia mwili wa marehemu
Askari wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga akishirikiana na msamaria mwema kusitiri mwili wa marehemu
Mwili wa marehemu baada ya kusitiriwa
Gari la polisi likiwasili eneo la tukio kuchukua mwili wa marehemu
Wananchi wakiwa eneo la tukio
Mamia ya wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio
Askari wa jeshi la polisi wakichukua mwili wa marehemu
Askari polisi wakiondoka na mwili wa marehemu
Askari polisi wakiondoka eneo la tukio
Wakazi wa Shinyanga wakiondoka eneo la tukio
Wakazi wa Shinyanga mjini wakiondoka eneo la tukio
Wananchi wakiondoka eneo la tukio baada ya polisi kuondoka na mwili wa marehemu
Jeshi la polisi mkoa wa shinyanga linawatafuta watu waliojichukulia sheria mkononi baada ya kumwua kwa kumpiga kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la mwatabora ,
tukio hilo la kusikitisha limetokea katika eneo la shinyanga mjini ambapo kijna huyo anatuhumiwa kuiba ndala ,
kamanda wa polisi mkoa wa shinyanga ametoa wito kwa wanainchi kushirikiana napolisi kuwakamata waliohusika katika tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment