KIKONGWE ALIYEKUTWA UCHI KWENYE NYUMBA YA MTU HUKO SHINYANGA AITAKA SERIKALI KUACHA KUKURUPUKA NA WAPIGA RAMLI.
SERIKALI
imeshauriwa kutekeleza kwa uangalifu mkubwa adhima yake ya kupambana na
waganga wa jadi wanaojihusisha na upigaji ramli zinazodaiwa ni chanzo
cha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albinism) kwa vile hatua hiyo
inaweza kusababisha madhara makubwa kwa taifa.
Ushauri
huo umetolewa na mmoja wa wazee maarufu mjini Shinyanga, Iddi Juma
ambapo amesema serikali haipaswi kukurupuka katika kushughulikia suala
la waganga wa jadi kwa vile baadhi yao wana umuhimu mkubwa kwa jamii na
wamekuwepo nchini tangu enzi na enzi.
Juma
alisema kuwadharau waganga wa jadi ni kutaka kusababisha matatizo
yasiyo ya lazima yanayoweza kutokea nchini kwa vile wengi wao wana uwezo
mkubwa wa kutibu baadhi ya magonjwa yaliyoshindikana kwa kutumia miti
shamba na hata baadhi ya viongozi wakubwa serikalini na wanasiasa
huwategemea waganga hao katika mambo yao mengi.
“Nimesikia
serikali imetangaza hivi karibuni itaendesha kampeni ya kupambana na
waganga wa jadi wanaopiga ramli chonganishi kwa kuwakamata na
kuwafikisha katika vyombo vya sheria, sipingani na kampeni hii, ombi
langu kwa serikali iwe makini inapotekeleza kazi hii vinginevyo inaweza
kutuletea madhara makubwa,”
“Waganga
wa jadi ni watu muhimu katika jamii yetu, kuna magonjwa
yanayoshindikana katika tiba za kitaalamu lakini wao wamekuwa
wakiyatibu, magonjwa mengine bwana hayana tiba katika hospitali zetu,
lakini ni rahisi mno kupata tiba yake kwa waganga wa jadi, kukurupuka na
kuwakamata ni kujiletea matatizo,”
"Hivi
kweli kuna tiba yoyote ya majini au mapepo machafu katika hospitali
zetu nchini? wanaopatwa na matatizo haya mara nyingi tunaona
wanakimbizwa kwa waganga wa jadi, ndiyo wataalamu wa kuyatibu, na huko
ni lazima mganga afanye mambo yake ili kubaini yametokea wapi, sasa
tukiwakamata wenye matatizo haya watatibiwa wapi?" alihoji Juma.
Mzee
huyo alisema yeye binafsi anao ushahidi baadhi ya viongozi wa kisiasa
na wa kiserikali ambao wanategemea sana nguvu ya waganga wa jadi, na
kwamba kutokana na hali hiyo ni wazi wale watakaokamatwa na kuchukuliwa
hatua watakuwa ni wasiokuwa na mahusiano na viongozi wowote ndani ya
serikali ama wanasiasa.
Alisema
yapo mambo yanayoweza kufanywa na waganga hao kutokana na kutoridhishwa
na hatua zitakazochukuliwa na serikali dhidi yao na hivyo kusababisha
mtafaruku mkubwa nchini ambapo amesisitiza umuhimu wa kutumika kwa
busara kubwa katika kuwabaini wanaojihusisha na upigaji ramli
chonganishi badala ya kukurupuka kukamata ovyo.
“Hawa
watu wasidharauliwe, maana wametajwa hata ndani ya vitabu vya mwenyezi
mungu, kwa sisi waislamu ipo aya inayoelezea jinsi mambo ya kichawi
yalivyofundishwa na malaika wawili, lakini mungu ametukataza kabisa
binadamu tusijihusishe nayo kwani ni fitina juu yetu, hivyo ni muhimu
tukawa makini katika kuwashughulikia,” alieleza Juma.
0 comments:
Post a Comment