Kesi inayomkabili kiongozi wa jumuiya na taasisi ya kiislamu nchini Sheikh Ponda Issa Ponda imeanza kusikilizwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro huku jeshi la polisi likilazimika kuwadhibiti wafuasi wa shekhe Ponda nje ya uzio wa mahakama.
Shahidi wa kwanza katika kesi hiyo ni aliyekuwa mkuu wa polisi
wilaya ya Morogoro (OCD) Sadick Tindwa ambaye kwa sasa ni OCD wilaya ya
Handeni mkoani Tanga ametoa ushahidi wake kwa zaidi ya saa mbili ambapo
ameieleza mahakama kuwa julai 31 mwaka 2013 akiwa OCD wilaya ya Morogoro
alipokea barua kutoka kwa umoja wa wahadhiri wa dini ya kiislamu
wakiomba kufanya kongamano la siku kuu ya Eid pili walilotaka kufanya
katika uwanja wa shule ya msingi kiwanja cha ndege manispaa ya Morogoro
Agosti 9 mwaka 2013 ambapo alitoa kibali kwa masharti ya kufanya
kongamano hilo kwa kutokutoa maneno ya kashfa dhidi ya dini nyingine.
Aidha amesema katika kongamaono hilo wahadhiri mbalimbali walitoa
mada ambapo msemaji wa mwisho alikuwa ni mshtakiwa Ponda Issa Ponda na
wakati akiendelea kuzungumza alitoa maneno yenye mitazamo ya uchochezi,
kashfa na kuumiza imani za dini nyingine ambapo amesema serikali
ilipeleka majeshi kwa wananchi wa Mtwara wakati walikuwa wakidai haki
yao kwenye gesi lakini kwa kuwa asilimia kubwa ya wananchi wa Mtwara ni
wasilaaam lakini serikali ilishindwa kupeleka majeshi kwenye mgogoro wa
loliondo kwa sababu asilimia kubwa ya wananchi wa lolindo ni
wakaristu.
Uchochezi mwingine umedaiwa kuwa shekhe Ponda aliwaambia waumini wa
kiisalaam wasiunge mkono kamati za ulinzi na usalama za dini kwani
zimeundwa na Bakwata pamoja na serikali kwa manufaa yao binafsi, hivyo
kamati hizo zikifika katika misikiti na kujitambulisha wafunge milango
na madirisha kisha wawapige.
Upande wa utetezi wenye mawakili watatu akiwemo wakili Juma Nasoro,
Batheromeo Tarimo na Abubakar Salimu wameuliza maswali ya msingi ambayo
ni: Je nafasi gani aliyokuwa nayo sheikh Ponda katika kongamano hilo?,
kuna uhusiano gani kati ya mashtaka aliyofunguliwa sheikh Ponda na
maneno aliyotoa kwenye kongamano?, kongamano lilikuwa halali ama sio
halali?, mbali na jamhuri je ni dini gani iliwahi kulalamikia kuumizwa na
maneno aliyotoa sheikh Ponda siku ya kongamanona ?
Kesi hiyo imeahiriswa na itaendelea kusikilizwa tena jan 27 mwaka huu katika mahakama ya hakim mkazi mkoani Morogoro.
0 comments:
Post a Comment