WATU WANNE WAFARIKI DUNIA BAADA YA KULA UGALI WENYE SUMU HUKO KIGOMA.
Watoto wanne wa familia moja wakazi wa kijiji cha kibambila wilayani Kakonko mkoani Kigoma wamefariki dunia na mmoja amelazwa katika kituo cha afya Kakonko baada ya kula chakula kinachosadikiwa kuwa na sumu.
Mganga
mkuu wa wilaya ya Kakonko Dkt. Fadhil Seleman amewataja watoto hao
waliofikishwa kituo cha afya Kakonko kuwa ni Neema Joseph, Jonas
Joseph, Majaliwa Joseph, Yusuph Joseph wote wakiwa na umri wa kati ya
miaka 11 na 18 walifikishwa hospitalini hapo wakiwa na hali mbaya na
walipoteza maisha wakati wanaendelea kupatiwa huduma.
Amesema kwamba uchunguzi wa awali umeonesha kuwa watu hao wamekula sumu katika chakula cha ugali.
Akizungumzia
tukio hilo baba wa watoto hao Joseph Kajolo ambaye alinusurika katika
tukio hilo amesema hajui chanzo cha tukio hilo huku baadhi ya wananchi
wa Kakonko wameeleza kusikitishwa kwao na tukio hilo na kwamba vifo vya
sumu katika wilaya hiyo vimekuwa vikijirudia mara kwa mara.
Mkuu
wa wilaya ya Kakonko Peter Toyima amesema polisi inamshikilia mtu mmoja
kuhusiana na tukio hilo huku akiwataka wananchi kuacha vitendo vya
kuwekeana sumu
0 comments:
Post a Comment