Mamlaka ya mawasiliano Tanzania Tcra inatarajia kuzima mitambo ya analogia mkoani Iringa na kuwasha ya digitali ikiwa ni mwendelezo wa kuzima mitambo hapa nchini.
akizungumza na mtandao huu naibu wa idala ya utangazaji tcra Fredrick Ntobi amesema kuwa kwa mara ya kwanza nchi hii kuingia katika mfumo wa digitali ilikuwa 31.12.2012 ambapo amesema walianza na mkoa wa dare-esalam na mikoa ya kanda ya ziwa na kufuatiwa mikoa mingine ambayo inaendelewa kuzi mwa mitambo hiyo.
aidha amesema kuwa hadi sasa wamekwisha toa elimu kwa jamii faida za kuingia katika mfumo huo wa digitali,
Hata hivyo amewatoa wasiswasi wanainchi mkoani iringa juu ya namna baada ya kuzimwa mitambo hiyo na kuwasihii kununua vingamuzi vitakavyo tumika na kwamba wamekagua maduka yote na kukuta vingamuzi vipo vya kutosha kwa wanainchi wote.
0 comments:
Post a Comment