BREAKING NEWS..!! WAZIRI WA NISHATI NA MADINI, PROFESA SOSPITER MUHONGO AJIUZULU.
Hatimaye Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospiter Muhongo amejiuzulu leo jijini Dar es Salaam.
Waziri Muhongo amechukua uamuzi huo leo ofisini kwake mbele ya waandishi wa habari.
Kujiuzulu
kwa Muhongo kumetokana na maazimio ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za
Serikali chini ya Mhe. Zitto Kabwe ilitokana na sakata la ufisadi wa
Akaunti ya Escrow ambapo zaidi ya shilingi bilioni 306 zilichukuliwa
kiholea Benki Kuu ya Tanzania na kusababisha mjadala mzito ndani na nje
ya Bunge.
Ukaguzi
maalum uliofanywa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na
uchuguzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwenye
akaunti hiyo, ulifanywa na ripoti zikatolewa na bunge, likajadili na
kufikia tamati kwamba kuna kodi ya umma iliibwa.
Kwa
vile suala hili liligusa utendaji wa viongozi wa ngazi za juu
serikalini pamoja na wanasiasa wengine, bunge lilitaka kuyumba kutokana
na kupendeleana licha ya ukweli kwamba fedha zilizochukuliwa ni nyingi
sana .
Ripoti
ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), chini ya Uenyekiti wa
Zitto Kabwe ilipitia kwa ufasaha ukaguzi wa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali,(CAG) na uchunguzi wa Takukuru wakatoa ripoti yao na
uthibitisho wa kutosha kuwa kuna (aliyekuwa) Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Jaji Frederick Werema, Waziri wa Madini na Nishati, Profesa
Sospiter Muhongo pamoja na watendaji wengine serikalini wamehusika kwa
njia moja au nyingine na upotevu wa fedha hizo za Escrow ama kwa
kukusudia ama kwa kutojua, kitu ambacho kilielezwa kuwa ni uzembe.
Rais
Jakaya Kikwete alichukua uamuzi wa kumfuta kazi Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kutokana na madai kuwa
alichotewa shilingi Bilioni 1.6 zilizotoka katika akaunti hiyo ya
Escrow.
Rais
Kikwete alisema Profesa Muhongo alikuwa amemuweka kiporo. Hata hivyo,
Watanzania wengi wakati wa kikao cha bunge liliopita walishangazwa kuona
baadhi ya wabunge kukaza misuli ya shingo zao na kutetea wizi ili
wahusika wasiwajibishwe. Wengine walipingana na ripoti ya CAG.
Wakati
wa kikao hicho cha Bunge aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji
Fredrick Werema alidaiwa kutaka kumpiga Mbunge wa Kigoma Kusini, David
Kafulila ambaye ndiye aliyeanzisha mjadala wa sakata hilo bungeni.
Vyombo
vya habari vikatangaza kuwa kama siyo kuzuiwa na mawaziri, Jaji Werema
angezua tafrani bungeni kutokana na kitendo chake cha kutaka kumpiga
mbunge huyo kutoka NCCR-Mageuzi, David Kafulila.
Ilidaiwa
kuwa tafrani hiyo ilitokea baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan
Zungu kuahirisha kikao cha Bunge hadi jioni ya siku hiyo, ikiwa ni muda
mfupi baada ya Werema na Kafulila kurushiana maneno bungeni baada ya
jaji kuchukizwa na kitendo cha mbunge huyo kijana kumwita mwizi, akijibu
mapigo baada ya mbunge huyo kuitwa tumbili (na mwanasheria mkuu huyo wa
nchi).
Waliomzuia
Jaji Werema asizipike baada ya kumzunguka inadaiwa ni baadhi ya
mawaziri ambao walimsindikiza hadi nje ya Ukumbi wa Bunge.
Jaji Werema pia
alituhumiwa kumtishia kifo Kafulila ambaye alilalamika bungeni. Ikadaiwa
kuwa jaji huyo alimtolea maneno hayo ya vitisho mbunge huyo kwenye
viunga vya bungeni mjini Dodoma baada ya bunge kuahirishwa.
Jaji Werema alinukuliwa
na vyombo vya habari akidaiwa kumwambia Kafulila: "I will take your
head, unless you apologize," ikimaanisha atamkata kichwa iwapo
hatamwomba msamaha!
Kufuatia tishio hilo
Kafulila akajihami kwa kuiandikia barua ya madai ya kutishiwa maisha
ofisi ya spika wa bunge, huku nakala ya barua hiyo akiipeleka kwa Mkuu
wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu na nakala nyingine
ameipeleka kwa kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma.
Hili ni tukio baya sana ambalo limeingia katika rekodi. Werema pia alijiuzulu kutokana na kashfa hiyo.
0 comments:
Post a Comment